Yanga yamtimua kocha wake Luc Eymael, TFF yamkalia kooni

27Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Yanga yamtimua kocha wake Luc Eymael, TFF yamkalia kooni

Uongozi wa Klabu ya Yanga umemfuta kazi Kocha wake Mkuu, Luc Eymael kutokana na kutoa kauli za kibaguzi na zisizo za kiungwana alizozitoa na kusambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari.

Luc Eymael.

Uongozi wa klabu hiyo umesema watahakikisha kocha huyo anaondoka nchini haraka iwezekanavyo.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema litamfikisha katika vyombo husika kocha aliyekuwa kocha wa Yanga Luc Eymael kutokana na matamshi yake ya kibaguzi kwa mashabiki wa timu hiyo pia imesema kuwa itamripoti kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Habari Kubwa