Wakati mashabiki wa Yanga walidhani wanaondoka na pointi tatu, mpira wa faulo uliopigwa kwenye lango la Yanga ulimgonga mikononi, Yassin Mustapha na mwamuzi kuamuru kuwa ni penalti, iliyowekwa wavuni kwa ustadi na Athanas aliyemuacha Metacha Mnata akiruka kushoto, mpira ukienda kulia.
Zilikuwa dakika nane za mwisho za kusisimua kwani ndizo zilizopatikana mabao yote mawili.
Dakika tano kabla ya pambano kumalizika, Yanga iliandika bao kupitia kwa Deus Kaseke, lililotokana na kujichanganya kwa mabeki wa Mbeya City na kumruhusu nyota huyo wa zamani wa wenyeji kufunga bao la utangulizi.
Kaseke ambaye jana alifikisha bao la tano msimu huu, aliudokoa mpira ulioserereka wavuni, licha ya juhudi na Salum Chitembe kuuokoa, lakini tayari ulikuwa umevuka mstari wa goli.