Yanga yatamba hesabu zitatimia

07Jul 2020
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe
Yanga yatamba hesabu zitatimia

LICHA ya timu yake kubanwa ugenini dhidi ya Biashara United, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amesema bado hesabu zake ni kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga inatarajia kushuka ugenini kesho kuikabili Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Akizungumza na gazeti hili jana, Eymael, alisema tayari ameshawaandaa wachezaji wake kutoidharau Kagera Sugar kutokana na ubora wa wachezaji waliokuwa nao na wakifahamu pia hawako kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Eymael alisema anahitaji kufikia malengo yake na amewaandaa wachezaji wake kupambana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Alisema kila mechi wanayocheza kwao ni muhimu licha ya kuwa tayari bingwa wa msimu ameshapatikana.

"Kuna mchezo dhidi ya Simba mbele yetu, ninajua hilo ila ni lazima tuanze kujipanga na mechi ambayo tuko nayo sasa, ni mchezo mgumu, Kagera Sugar haitakuwa tayari kufungwa kwa mara nyingine," Eymael alisema.

Aliongeza kila mchezaji anajua wanahitaji kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa na ili wafike huko, ni lazima washinde mechi zote zilizobaki.

"Kagera Sugar ni mechi ya ushindani, kwa sababu wanahitaji kulipa kisasi, hawatakuwa tayari kufungwa tena ndani ya siku chache, tutaingia uwanjani tukiwaheshimu wapinzani wetu," Mbelgiji huyo alisisitiza.

Alieleza mbali na ushindani, wanatarajia pia mchezo huo utakuwa na burudani kwa sababu ya ubora wa kiwanja watakachochezea.

"Tunajipanga kumaliza jukumu la kuifunga Kagera Sugar, halafu tuendelee na mikakati ya kuwamaliza Simba, tunahitaji kuchukua kikombe cha FA kuliko

Alisema wanatakiwa kumaliza na Kagere kuhakikisha wanapata alama muhimu ili waendelee na maandalizi ya mechi ya nusu fainali.

Habari Kubwa