Yondani kuwavaa waarabu

09Aug 2016
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe
Yondani kuwavaa waarabu

BAADA ya kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili beki Kelvin Yondani ameanza mazoezi na timu hiyo na yupo tayari kuwavaa waarabu Jumamosi.

beki Kelvin Yondani.

Yondani aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Medeama ya Ghana kwenye mchezo wa kundi A kombe la Shirikisho.

Yondani aliukosa mchezo wa juzi wa kirafiki kati ya Yanga na Mtibwa Sugar uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema nyota huyo ameanza mazoezi na kikosi cha timu hiyo na kuna uwezekano wa kucheza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mo Bejaia.

"Amepona kabisa kwa sasa na juzi alianza mazoezi..,kocha anendelea kumfuatilia kuona kama anaweza kucheza Jumamosi," alisema Saleh.

Mchezo huo wa Jumamosi kombe la Shirikisho Afrika utakuwa wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Algeria, Yanga walilala kwa goli 1-0.

Habari Kubwa