Zahera apagawa majembe mapya

10Dec 2018
Faustine Feliciane
DAR ES SALAAM
Nipashe
Zahera apagawa majembe mapya

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kwa usajili wanaoufanya katika dirisha hili dogo, ana uhakika wa kuendelea kufanya vizuri msimu huu, kwa kuwa mapendekezo aliyoyatoa kwa uongozi yanafanyiwa kazi kama alivyotaka.

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera,

Akizungumza na Nipashe jana, alisema matumaini ya kikosi chake kuendelea kutisha anayapata pia kutokana na sapoti kubwa anayoipata kutoka kwa uongozi hadi mashabiki.

"Nilihitaji winga kuongeza makali, uongozi umenisikiliza, naamini kwa mambo yanavyokwenda tuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri," alisema Zahera.

Aidha, alisema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakimuunga mkono uwanjani kwa matokeo mazuri wanayoyapata.

"Kikosi changu kina mapungufu, lakini wachezaji wangu wamekuwa wakijatahidi kuyaficha, wanapambana uwanjani, ujio wa wachezaji wapya utatuongezea kitu," alisema Zahera.

Yanga imemsajili winga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na usajili huo ukitokana na mapendekezo ya Zahera.

Yanga pia inampango wa kumsajili golikipa kwa ajili ya kuimarisha nafasi hiyo kwenye kikosi chao.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya klabu hiyo, Hussein Nyika, alisema kuwa wanachofanya ni kutekeleza mapendekezo ya kocha wao.

"Tuna kocha mzuri, tunachofanya ni kutekeleza mapendekezo yake…, bado tunaendelea na usajili kwa nafasi ambazo kocha ameshauri," alisema Nyika.

Habari Kubwa