NDANI YA NIPASHE JUMAPILI

Asha Ibrahimu ambaye ni mlemavu wa miguu, mkazi wa kijiji cha Unyabwa, Manispaa ya Singida, akilia mbele ya Mkuu wa Mkoa Singida, Peter Serukamba, baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja alichosotea kwa miaka 25 kufuatilia ofisi mbalimbali za serikali hadi Rais Samia Suluhu Hassan alipoamuru apewe kiwanja haraka. PICHA: THOBIAS MWANAKATWE

Fundi wa TANESCO, akikagua mita ya umeme kwa mteja ili kuwabaini waliounganishia huduma kinyemela kwa kutumia mafundi vishoka kupitia huduma bila malipo katika Kata ya Isagehe, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga jana. Kulia ni moja ya mita mbovu iliyoibwa katika shirika hilo, na kukutwa ikiwa imefungwa katika Kanisa la Kalval Assembel of God (ACG), huku nyaya zinazoruhusu mita kusoma zikiwa hazijaunganishwa na kuruhusu umeme kuingia moja kwa moja kwa mteja. PICHA: SHABAN NJIA