NDANI YA NIPASHE LEO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Ali Suleiman (wa tatu kushoto) akimlisha keki maalum Mwenyeki wa bodi ya Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), Ramadhani Mwalimu Khamis (wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya kulipongeza shirika hilo kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake wakati wa hafla maalum iliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ZIC, Arafat Haji (wa pili kushoto), Naibu Kamishna Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Said (Kulia) na Mkurugenzi wa Bima ya Kawaida wa ZIC, Jape Khamis (Kushoto)

Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori (kushoto), akibadilishana mkataba na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk. Benson Ndiege, baada ya hafla ya kusaini makubaliano hayo kati ya ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na NMB wa kujenga maghala kwenye vyama vya ushirika, jana jijini Dodoma. PICHA: MPIGAPICHA WETU