Magari kupunguza uchafuzi wa mazingira yazinduliwa

02Dec 2018
Gwamaka Alipipi
Dar es Salaam
Nipashe
Magari kupunguza uchafuzi wa mazingira yazinduliwa

SHIRIKA la Scania Tanzania limezindua aina mpya ya malori ambayo hayataleta athari kwenye uchafuzi wa mazingira nchini, pamoja na kumsaidia dereva kuendesha kwa usalama na ufanisi zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Scania, Lars Eklund alisema Tanzania inahitaji usafiri ambao utapunguza athari kwenye mazingira na kuleta faida za kiuchumi,

“Ustawi pia ni usalama wa barabarani, tunahitaji kupunguza ajali kwa manufaa ya binadamu, kwa jamii na kwa manufaa ya biashara, mambo haya daima huenda kwa mkono kwa mkono, faida na ustawi,” alisema Eklund.

Meneja mauzo wa magari kutoka Shirika la Scania Tanzania, Martin Luther alisema malori hayo yamepunguzwa kwa asilimia 70 utoaji wa hewa chafu.

Alisema injini yake ni nyepesi ikiwa na kilo 100, pia yanatumia kiasi kidogo cha mafuta, ambapo umbali wa kilometa moja inatumia mafuta lita tatu na nusu.

 

 

Habari Kubwa