Njaa inakuja Burundi, Zimbabwe imeshafika

09Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Njaa inakuja Burundi, Zimbabwe imeshafika

HALI mbaya ya hewa, joto kuongezeka kumeleta athari nchini Burundi kuna shaka ya kuathiri kiwango cha uzalishaji chakula katika nchi hiyo.

Wataalamu waliokuwa jijini Geneva, Uswisi wanasema, joto hilo limevuruga mfumo wa uzalishaji chakula na upatikanaji wake, shida kubwa ni hali ya hewa. 

Inaelezwa kitaalamu kwamba, katika orodha ya nchi 10 ambazo ziko hatarini kuvuna chakula kidogo duniani, inatoa kwa kiasi kikubwa hewa ya ukaa ambayo ina athari katika uzalishaji.

Katika hilo zinatajwa nchi tano katika ngazi ya juu ya hali mbaya zaidi ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Madagascar, Yemen na Sierra Leone.

Hapo zinafuatiwa katika orodha hiyo, na Chad, Malawi, Haiti, Niger na Zambia.

"Watafiti wetu wanaonyesha kuingzeka hewa ya ukaa angani inayoendana na kupungua tija ya chakula tunachokula, tukiwa ni watu tunaoumia zaidi na hili na ongezeko la hea ukaa,” anasema Dk. Samuel Myers, Mtafiti Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani.

Pia, kuna maoni ya watafifi wengine kwamba, ripoti yha kutokuwa na uhakika wa chakula, inawagusa matajiri na masikini, kwamba athari ya hali ya hewa inaendana moja kwa moja na uwezo wa jamii kujilisha

Mtaaluma Profesa Doreen Stabinsky, anahimiza kwamba vigezo vilivyopo vinaashiria hali si nzuri na kuna haja ya kuchukuliwa hatua 

Wakati inaelezwa Burundi imo katika nafasi ya ‘kumi bora,’  ndugu zao wa Zimbabwe kumeshaharibika kwa watu zaidi ya milioni tano wamekumbwa na njaa na wanaendelea kutaabika.

Taarifa ya Umoja wa Taifa, inakiri hali ni mbaya, huku Mpango wa Chakula Duniani (WFP), imeanzisha kazi ya kukusanya Dola za Marekani milioni 331 kuwaokoa waathirika.

Mkuu wa shirika hilo, David Beasley, anasema suala hilo linapaswa kufanyiwa kazi katika mtazamo wa dharura.

Hiyo inaelezwa kwamba hali iliyotokea ni zao la ukame uliochukua sura katika nchi hiyo, huku bei ya  mazao ikipanda maradufu.

Pia, kiwango cha maji kushuka katika maeneo ambako kunazalishwa umeme katika |Bwawa la Kariba na kupoteza umeme, ikizaa athari nyingine ya kiuchumi na kijamii.

Habari Kubwa