Lugola aonya polisi wanaoshiriki uhalifu

10Aug 2019
Friday Simbaya
IRINGA
Nipashe
Lugola aonya polisi wanaoshiriki uhalifu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepokea msaada wa pikipiki mbili aina ya ‘Boxer’ zenye thamani ya Sh. milioni 2.8 kwa ajili ya Jeshi la Polisi mkoani Iringa huku akionya askari wa jeshi hilo kushirikiana na wahalifu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola

Msaada huo wenye lengo la kupambana na uhalifu kwenye maeneo  korofi ya Ikokoto na Mlima wa Kitonga wilayani Kilolo, umetolewa na Mbunge wa Kilolo, Venance  Mwamoto (CCM).

Lugola alisema pikipiki hizo zisitumike kwa uhalifu kama vile kusindikiza mirungi na badala yake zitumike kwa ajili ya malengo yaliokusudiwa.

Waziri huyo alipita mkoani humo na kutoa maelekezo ya kiutendaji wakati akielekea Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

“Tumepokea pikipiki hizi, naomba  askari watunze ili zidumu, zitumike kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo korofi hususani maeneo ya Mlima Kitonga wilayani Kilolo,” aliagiza.Lugola pia alitoa wito kwa wananchi na wadau kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kulipatia misaada na taarifa za uhalifu.

Habari Kubwa