Guardiola: VAR imebadilisha nguvu ya mchezo

12Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
LONDON, England
Nipashe
Guardiola: VAR imebadilisha nguvu ya mchezo

KOCH wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kwamba, matumizi ya teknolojia ya usaidia wa maamuzi kwa njia ya video,VAR, hubadilisha "nguvu" ya michezo baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya West Ham juzi Jumamosi, ambapo mshambuliaji Gabriel Jesus-

Pep Guardiola

-alikuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu bao lake kukataliwa.

Wakati wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0, Jesus alifunga bao lililodhaniwa kuwa ni la tatu kwa City, lakini mwamuzi, Mike Dean alilikataa bao hilo kuwa ni la kuotea baada ya kuitumia VAR.

Huu ni msimu wa kwanza teknolojia hiyo kutumika kwenye Ligi Kuu ya England na VAR ikatumika tena kwenye mchezo huo, wakati penalty ya Sergio Aguero ilipookolewa na kulazimika kuipiga tena.

"Unatakiwa kuwa imara kialiki wakati VAR inapokuwa haipo upande wako," alisema Guardiola akiiambia BT Sport.

"Unafikiri kwenye mchezo unaongoza kwa 3-0, lakini kumbe matokeo yanasema 2-0, kwa hakika mchezo unakuwa tofauti kabisa.

"Unatakiwa kuwa mtulivu na imara. Inakwenda kubadilisha nguvu sio tu kwa timu, lakini pia kwa watangazaji. Litakuwa somo zuri kwa siku zetu za usoni."

VAR ilikuwa sababu kubwa ya City kutolewa kwenye ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita, maamuzi ambayo yalikataa bao la dakika za mwisho la Sterling ambalo lingewapeleka robo fainali dhidi ya Tottenham.

"Baada ya kile kilichotokea kwenye mchezo dhidi ya Tottenham kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, kwa sasa angalau tunaweza kutuliza hisia zile," amesema Guardiola.