De Gea bado hakijaeleweka Man United

12Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
MANCHESTER, England
Nipashe
De Gea bado hakijaeleweka Man United

GAZETI la The Mirror limebainisha kwamba majaliwa ya golikipa wa Manchester United, David de Gea bado yapo shakani.

David de Gea

Gazeti hilo limedai kwamba, raia huyo wa Hispania bado hajakubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukaa hapo kwenye dimba la Old Trafford.

Mapema mwezi uliopita ilidaiwa kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 28 amekubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ambao unamfanya alipwe kiasi cha pauni 350,000 kwa wiki.

Lakini taarifa za sasa zinasema kwamba, mazungumzo hayo hayakuweza kufikia makubaliano kati ya wawakilisha wa de Gea na maafisa wa Man United.

Hivyo basi ESPN FC imeripoti kuwa klabu kubwa Ulaya kama Paris Saint-Germain na  Real Madrid zitaingia tena sokoni kwa ajili ya kuwania saini ya kipa huyo.

Kipa huyo wa zamani wa klabu ya Atletico Madrid, de Gea atakuwa huru kuzungumza na klabu yoyote mwishoni mwa mwaka huu na anaweza kusaini makubaliano ya awali na kumfanya kumuacha kocha Ole Gunnar Solskjaer kulazimika kuingia tena sokoni kipindi kijacho chamjaira ya joto.

Habari Kubwa