Salma Kikwete awataka wazazi kusomesha watoto

13Aug 2019
Said Hamdani
LINDI
Nipashe
Salma Kikwete awataka wazazi kusomesha watoto

WAZAZI na walezi katika  mikoa ya Lindi na Mtwara, wametakiwa kuwahimiza watoto wao kwenda shule wapate elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.

mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Salma Kikwete

Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na mke wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Salma Kikwete, alipokuwa akitoa salamu kwa wananchi waliojitokeza katika kilele cha Siku ya Wakulima, Nanenane Kanda ya kusini katika Manispaa ya Lindi.

Salma pia aliwashauri wazazi kuwaelimisha watoto wajiepushe na mimba za utotoni ili kufikia ndoto zao.

Salma ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, alisema wasichana wanapopata mimba wakiwa na umri mdogo, hali hiyo inawasababishia athari kubwa ikwamo kuwakatishia ndoto zao za baadae.

“Ninawaomba sana wazazi wenzangu wa Lindi na Mtwara, hakikisheni mnawapeleka shule wakape Elimu watoto wenu,” alisema.

Pia, aliwakumbusha wananchi wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura ili waweze kuitumia demokrasia yao ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.