Rai kwa wanahabari kuelimisha jamii uvamizi malori ya mafuta

14Aug 2019
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Rai kwa wanahabari kuelimisha jamii uvamizi malori ya mafuta

Kuwepo na kushamili kwa matukio mengi ya ajali za malori vyombo vya habari nchini vimeobwa kuwa na vipindi maalumu vya kuelimisha jamii athari za kuvamia malori ya mafuta yanapopata ajali pamoja na kuchota mafuta.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko

Wito huo umetolewa jijini hapa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko, na kusema akumbukumbu zinaonyesha kuwapo kwa matukio mengi ya ajali za malori kupata ajali na wananchi kufariki walipokuwa wanachota mafuta.

Alisema, matukio kama hayo yalitokea mwaka 1998 lori la mafuta lilipata ajali eneo la Isongole Mbeya na watu walifariki dunia wakiwa kwenye harakati za kuchota mafuta, 2008 eneo la Mdaula Chalinze karibu na Morogoro, 2010 eneo la Manyoni 2013, eneo la Mbagala jijiji Dar es Salaam na la Jumamosi  eneo la Msamvu mkoani Morogoro.

"Mtiririko wa matukio haya unatia shaka na kutuaminisha kuwa hakuna elimu ya kutosha juu ya athari za vitendo vya kuvamia malori na kuchota mafuta yanapopata ajali, hivyo ni muda mwafaka kwa vyombo vya habari kutoa uchechemushi na kuelimisha jamii juu ya jambo hili, pia tunato pole kwa ndugu zetu, Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali  ya Msamvu na majeruhi wapone na kurejea katika shughuli zao za kila siku,” alisema Soko.

Pia alivitaka,vyombo vya habari kuacha mara moja kuchapisha picha zenye ukakakasi (kutumia picha ya maiti iliyo haribika) kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja misingi ya uandishi wa habari na kuchochea maumivu kwa msomaji.

“MPC inawakumbusha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini hasa wanaofanya kazi ya kuchapisha, kutangaza na kurusha habari katika mitando ya kijamii (Online journalism) kuzingatia weredi na taaluma katika kupiga picha za miili ya marehemu walio ungua katika ajali,” alisema.

Aidha, baada ya kutokea kwa tukio la ajali hiyo MPC imefanya tathimini ya namna vyombo vya habari vilivyochapisha habari hiyo ikiwamo magazeti, radio, luninga na mitandao ya kijamii na kushuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye vyombo hovyo, jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na upashaji habari kwa njia ya picha.

"Kwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano na Posta (maudhui ya mtandaoni) Epoca 2018 kifungu cha 5(1) a,b,c,d,e, na f,endapo utakiuka vifungu vilivyoaninishwa katika sheria hiyo basi utakuwa umetenda kosa na unaweza kutozwa faini sio chini ya shilingi million tano au kifungo kisichopungua miezi kumi na miwili,"alisema.

Aliwataka waandishi wa habari kutimiza vyema majukumu yao ya msingi ya kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha, kuonya sanjali nakufanya ukosoaji jengefu bila kuvunja maadili pamoja na kuwa mabalozi wa kuieleimisha jamii kutumia vyema mitandao ya kijamii hasa uandishi wa kiraia.

Habari Kubwa