Tamasha la jinsia laja kuikomboa upya jamii

30Aug 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Tamasha la jinsia laja kuikomboa upya jamii

TUNAPOZUNGUMZIA tamasha, huo ni mkusanyiko wa watu kutoka makundi mbalimbali.

Matamasha mara nyingi yanasaidia watu wa sehemu moja kuungana na watu wale sehemu nyingine na baadaye wanakuwa kitu kimoja.

Pia, yanawasaidia watu kujifunza  mengi kupitia ushiriki wao. Hapo ndipo panasemwa “mnakutana na kubadilishana mawazo.”

Katika tamasha ndiko mtu anapata fursa ya kushiriki na kwa sababu atanufaika na kuyajua mambo mengi.

Hivyo, wanajamii inatakiwa kuwa mbele wanaposikia tamasha wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kunufaika na chochote ambacho kitazungumzwa katika tamasha hilo.

Mwezi huu, asasi ya TGNP Mtandao inatarajia kufanya tamasha kubwa litakalokusanya zaidi ya watu 1,500 kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi. Ni sehemu ya hatua ya asasi hiyo kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.

Hivyo, kuna mada mbalimbali zitakazojadiliwa, zote zikiwa na ujumbe wa kuisaidia jamii kokote iliko, katika sura pana ya kufahamu tulikotoka na tunakoelekea.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TGNP Mtandao, Monica John, tamasha hilo litazungumzia masuala ya utekelezaji wa maudhui ya ajenda ya Mkutano wa Beijing na kufanya mikakati ya pamoja kuona wapi tunaenda na wapi tuliko.

Monica anasema, tamasha la jinsia linaimarisha ujenzi wa nguvu za pamoja katika umoja wao kupaza sauti.Kutokana na umuhimu wake, umma kutoka mikoa mbalimbali na nchi mbalimbali utakusanyika kushiriki kwenye tamasha hilo.

Anaongeza kuwa tamasha hilo la 14 kwa mwaka huu litafanyika mwezi ujao kuanzia tarehe 23 hadi 27, ambayo hasa ni kipindi cha umri miaka 25 ya TGNP Mtandao inatimizwa, vivyo hivyo kwa azimio la Mkutano wa Beijing.

Monica anasema, malengo ni kutafakari na kupeana taarifa, kisha kujifunza ili kuweza kuzitambua nyanja mbalimbali husika, mada kuu ni harakati za wanawake zinavyoweza kuleta mabadiliko.

Amina Juma, mmoja wa washiriki wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS), anasema tamasha hilo limekuja kwa wakati na litawasaidia washiriki kujua mengi kuhusu ukatili wa kijinsia katika sura pana.

Mama huyo anahimiza kwamba, kupitia tamasha hilo washiriki watabadilishana mawazo na makundi mbalimbali na hivyo anashauri jamii, ijitokeze kushiriki tamasha hilo ili inufaike kupitia mada zitakazojadiliw

Habari Kubwa