KCB yaimwagia Ligi Kuu Bara mil. 495/-

05Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
KCB yaimwagia Ligi Kuu Bara mil. 495/-

LIGI Kuu Tanzania itazidi kunoga na kuongezeka ushindani kufuatia Benki ya KCB Tanzania kuingia mkataba na Shirikisho la Soka nchini (TFF) wa kuwa mdhamini mwenza katika msimu huu wa 2019/20.

KCB Tanzania sasa inaungana na Kampuni ya Vodacom ambayo ni mdhamini mkuu baada ya mwezi uliopita kampuni hiyo ya mawasiliano kuingia mkataba na TFF wa kuidhamini ligi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu kwa thamani ya Sh. bilioni tisa.

Kwa upande wa KCB, mkataba wao una thamani ya Sh. milioni 495.6 kabla ya kodi, na ulitiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Cosmas Kimario na Rais wa TFF, Wallace Karia katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam jana na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania, John Ulanga, Katibu Mkuu TFF, Kidao Wilfred, Mwenyekiti wa Bodi

ya Ligi Kuu, Steven Mnguto na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi,  Boniface Wambura pamoja na Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania.

Hii ni mara ya tatu kwa KCB Tanzania kudhamini ligi hiyo, mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 2017/18 ambapo ilidhamini Ligi Kuu kwa Sh. milioni 325 na kuongeza udhamini kwa msimu uliofuata wa 2018/19 hadi kufikia Sh. milioni 420.

Akizungumza katika halfa ya utiaji saini mkataba huo jana, Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa udhamini wa misimu iliyopita ndiyo yameivutia  KCB Tanzania kuendeleza udhamini

huo na kuwa Sh. milioni 495.6

ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia msimu wa 2017/18 hadi 2019/20 udhamini wao utakuwa jumla ya Sh. bilioni 1.16.

Kimario alisema pamoja na

dhamira ya benki hiyo kurudisha kwa jamii, udhamini huo pia ni fursa kubwa kwa KCB kuwekeza kwenye sekta yenye kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza ajira na

vipaji vya vijana wa Kitanzania.

“Matarajio ya benki yetu ni kuona Watanzania wengi zaidi

wanapata ajira kupitia sekta mbalimbali tunazozigusa, ” alisema.

Rais wa TFF, Karia mbali na kuishukuru KCB Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Bara, alisema udhamini wao utasaidia kufanikisha msimu huu wa 2019/20 huku akizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo.

Habari Kubwa