… Awataka wahandisi kupunguza gharama

05Sep 2019
Mary Geofrey
DAR ES SALAAM
Nipashe
… Awataka wahandisi kupunguza gharama

RAIS John Magufuli amewataka wabunifu na wakadiriaji majenzi, kushusha gharama za uchoraji ramani ili Watanzania waweze kumudu kutumia huduma
hizo nchini.

Rais Magufuli alitoa wito huyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua  mkutano wa pamoja wa bodi za Usajili wa WabunifuMajengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Usajili wa Wahandisi (ERB) naUsajili Makandarasi (CRB).

Alisema wataalam hao wamekuwa wakitoza gharama kubwa za ramani hadi Sh. milioni mbili wakati ramani zenyewe wanazichukua kwenye mitandao ya intaneti.

“Nawasihi mpunguze gharama za kuuza ramani za nyumba ili mpate watejawengi kwa sababu ramani mnauza kuanzia Sh. milioni mbili, wakatimwingine mnazi’google’ kwenye mitandaoni alafu mnamtumia mtu hadi tatu achague lakini mnauza gharama kubwa,” alisema Rais.

Alisema gharama ya Sh. milioni mbili ni kubwa hivyo Watanzania wengihawawezi kumudu hivyo ni muhimu kuzishusha.

Aidha, Rais Magufuli alizitaka bodi hizo kuendelea kuongeza ukali nakuchukua hatua kwa watendaji ambao hawatimizi wajibu wao kikamilifuikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni zao.

Alisema licha ya watalaam wanaokiuka taratibu kuchukuliwa hatuachangamoto iliyopo ni makandarasi wanaofukuzwa kusajiliwa kwa majinamengine.

“Kama ni kufukuzwa kazi afukuzwe kabisa, akafuge samaki, msiwa‘entertain’ (msiwaendekeze’), kuwe na kampuni chache zinazofanya kazivizuri kuliko kuwa na nyingi zisizo na tija,” Rais Magufuli alisema.

Kadhalika Rais Magufuli aliagiza watendaji wa bodi hiyo kwakushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kubadili sheria ambazozinawabana makandarasi na wataalam hao wa ndani kufanya kazi za miradimikubwa.

Alisema mbali na upungufu ya kisheria makandarasi wengi hawanaudhubutu wa kuomba tenda na wengine huingia mitini kabla hawajamalizakazi.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Consolata Ngimbwa, aliiomba serikali kuweka mazingira wezeshi ya kisheriaya utekelezaji wa miradi ya serikali ili makandarasi wa njekushirikisha makandarasi wa ndani katika kazi zao.

“Tumejitahidi sana kuwaunganisha makandarasi wetu kwenye miradimbalimbali mikubwa inayojengwa na wageni lakini kwa sababu hakunasheria inayowalazimu kutoa kazi kwa wazawa ni kuomba na wanaoombwawanatoa wanavyojisikia na hata malipo wanayotoa si mazuri sana, kwahiyo tunaomba utusaidie hili ili miradi ijayo tushiriki vizuri,"alisema Ngimbwa.

Alisema pia watendaji wengi wa serikali kutoa uhuru kwa makandarasikutumia benki na bima badala ya wao kulazimishwa kutumia benki tu na kwamba wanaomba miradi iongezeke ili lengo la kukuzamakandarasi litimie kwa sababu miradi wanayopewa ni michache.

MGOGO AIBUA SHANGWE

Katika hatua nyingine Mchungaji Mashuhuri nchini, Daniel Mgogo, janaalizua taharuki nashangwe katika mkutano huo.

Mchungaji Mgogo alizua taharuki hiyo kwa kushangiliwa na washirikikatika mkutano huo zaidi ya 4,000, baada ya kuitwa na mshehereshaji kwa ajili ya kufanya maombi kabla ya kuanza mkutano huo.

Mchungaji Mgogo alitanguliwa na viongozi wengine watatu wadini akiwamo Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salumna makasisi wawili wa Kanisa Katoliki na Anglikana.

Alipoitwa m Mchungaji Mgogo, watu walilipuka kwa shangwe na kuanzakumfurahia wakati akielekea mbele kwa ajili ya kusoma dua hiyo.

Kutokana na shangwe hizo, Mchungaji Mgogo alianza kwa kumwomba msamaha Rais Magufuli kwa kile kinachotokea huku akimweleza kuwa niudhihirisho kuwa ana wafuasi wengi wanaofuatilia kupitia mitandao yakijamii.

Mchungaji Mgogo alianza kwa kumsifia Rais John Magufuli kwa kazi nzurianazofanya na kusema kuwa Watanzania wapo nyumba yake na wanazikubali.

“Rais Magufuli acha niseme tu hii fursa niliitafuta muda mrefu, achanikueleze tu kuwa tumekuelewa, hata kama wahawajasema lakiniwanakuelewa," Mchungaji Mgogo alisema.

Habari Kubwa