Sakata kupinga nyama  latinga Mahakama Kuu

05Sep 2019
Nipashe
Sakata kupinga nyama  latinga Mahakama Kuu
  • Shauri la kurasa 400, mwanasheria korti ‘hoi’

MWANAMKE nchini Australia, amewafikisha mahakamani majirani zake akidai kukerwa na uchomaji nyama katika eneo la nyumba yake.

Jiko kunakoandaliwa mishikaki.

Cilla Carden, kutoka jiji la Perth, Magharibi mwa Australia, amedai kuwa shughuli zao za uchomaji nyama, uvutaji wa sigara na kelele za watoto unavunja sheria za makazi ya watu.

Amefuata njia hiyo ya kisheria, ili shughuli hizo ziache kufanywa na majirani.

Hata hivyo, ni shauri lililochukua mkondo mrefu kisheria, sasa ikitinga katika Mahakama Kuu, baada ya mchuano na maamuzi ya awali kutofikia maafikiano sahihi.

Mahakama ya Jimbo, imetupa mbali madai yake kwa kusema kuwa hayana maana na ushahidi wa kutosha.

Mjadala wa hoja hiyo kizimbani, yalihusisha maelezo kama familia zinazoishi jirani yake kupunguza mwanga wa taa zao, kuwanyamazisha wanyama wanaofuga, pamoja na kuweka miti kwenye bustani zao za mapumziko.

Anasema kuwa, harufu ya moshi wa sigara na nyama choma, zimemsababishia ashindwe kuishi vizuri.

''Siwezi kufurahia sehemu yangu ya kupumzika. Wameweka jiko la nyama choma ili nifikiwe na harufu ya samaki - harufu pekee ninayopata ni ya samaki tu,'' anasema Cilla Carden, Jumatatu wiki hii.

Mahakamani alijibiwa kuwa familia hizo zinajaribu kuishi kama pamoja, Hata hivyo familia waliyokua wakilalamikiwa, wameshahamisha jiko lao la kuchomea nyama, kama sehemu ya kumsaidia mlalamikaji.

Mahakama iliongeza pia, familia hiyo wamekua hawawashi taa usiku na kuwazuia watoto kucheza kutokana na hofu walioipata kwa kushitakiwa.

Mama Carden alikata rufani kuhusu uamuzi huo katika Mahakama Kuu ya Australia Magharibi, alikabidhi kurasa zaidi ya 400 zenye malalamiko ya kukata rufani mwezi Machi.

Mwanasheria Mkuu wa Mahakama hiyo, anadai kuwa kurasa 400 zilikabidhiwa kwa mahakama zinashangaza an anongeza:

"Hawaruhusu watoto wao kutoka nje usiku. Hawajawasha taa kwa siku kadhaa wakiogopa hatua atakazozichua mlalamikaji na jirani yao. Hili halikubaliki."

Mwezi Julai mahakama iliamua dhidi ya mlalamikaji wakisema malalamishi yake yamekuwa mzigo mzito kwa majirani, huku mlalamikaji Carden akiwajibu kuwa atachukua hatua zaidi katika mahakama nyingine.

Habari Kubwa