Kulikoni Siku Wafanyakazi Marekani ni Septemba?

06Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kulikoni Siku Wafanyakazi Marekani ni Septemba?

KWA Wamarekani, Siku ya Wafanyakazi kama ilivyo sehemu nyingine nyingi ni ya kitaifa, iliyoanzishwa kuwaenzi wafanyakazi wa Marekani na michango yao katika uchumi,wakisherehekea mwezi Septemba.

Wamarekani wakisherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi.

Ni tofauti na sehemu nyingi duniani, ikiwamo Tanzania wanakosherekea siku ya Mei Mosi ya kila mwaka.

Wamarekani wengi wanaitumia siku hiyo kuadhimisha kumalizika kwa kipindi cha joto, hapo ndipo inapojenga suala la kustaajabu juu ya chimbuko hilo linalotokana na harakati za wafanyakazi mwishoni mwa mwaka 1800.

Ilikuwa wakati wa mapinduzi ya viwandani yamefikia kileleni, Wamarekani walifanya kazi kwa saa 12 kwa siku, katika siku zote saba kwa wiki ndani ya katika mazingira magumu na malipo duni.

Hata watoto wadogo walikuwa wanafanya kazi viwandani. Karibu kila mwajiri hakutoa likizo ya ugonjwa kwa wafanyakazi, likizo ya kawaida au maslahi ya afya.

Kadri walivyoendelea kujipanga zaidi katika vyama vya wafanyakazi, walianza kwa  kuandamana kupinga hali mbaya na hatarishi za maeneo ya kazi na kushawishi maslahi zaidi kutoka kwa waajiri.

Hatua hiyo ya kuwatambua wafanyakazi kwa kuwapa likizo, ilianza kwa serikali za majimbo zikipitisha sheria za kumjali mfanyakazi wa kawaida.

Bunge la Marekani lilianzisha sikukuu ya wafanyakazi kitaifa mnamo Juni 28, 1894, na kuweka Jumatatu ya kwanza ya mwezi Septemba kuwa Siku ya Wafanyakazi.

Tofauti yake  na Siku ya Wafanyakazi ya Mei Mosi inaadhimishwa zaidi katika nchi zenye viwanda ulimwenguni.

Mnamo Mei 1886, maandamano ya wafanyakazi yalifanyika katika bustani ya Haymarket iliyoko Chicago, kushinikiza kazi zifanywe kwa saa nane.

Bomu lililipuka katika maandamano hayo na kumuua ofisa wa polisi na raia wanne. Ni tukio lililofanya habari hiyo kuvuma duniani kote na maadhimisho ya kila mwaka ya maandamano ya wafanyakazi, duniani.

Kwa nini hawaadhimishi Mei Mosi? Upinzani mkubwa dhidi ya harakati za umoja wa wafanyakazi uliibuka nchini Marekani.

Baada ya miaka kadhaa, Mei Mosi ikawa inanasibishwa na siasa za mlengo wa kushoto, wakati Siku ya Wafanyakazi, ilikuja kuongezeka kutambuliwa na manispaa na majimbo.

Wakati Marekani ilidhamiria kuanzisha sikukuu ya kitaifa ya wafanyakazi, Rais wake Grover Cleveland, hakutaka kuchagua siku ya tarehe halisi ya Mei Mosi, kwa sababu ya kuhusishwa siku hiyo na mlipuko wa bomu huko Haymaker,  badala yake akachagua mbadala wa Septemba.

Habari Kubwa