Usalama barabarani yatamba kupunguza ajali

06Sep 2019
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Usalama barabarani yatamba kupunguza ajali

TAKWIMU zilizotolewa ndani ya 24 kwa nchi nzima zinaonyesha kuwa ni ajali mbili pekee zimetokea katika mikoa ya Kigoma na Katavi.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilim,

Akitoa takwimu hizo Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilim, alisema kwa majeruhi wa ajali za magari tangu Januari hadi Julai 2018 ilikuwa  2381, wakati Januari hadi Julai, mwaka huu zimetokea ajali 1,741.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha kufanikiwa kupunguza ajali 640 ambazo ni sawa na asilimia 27.

Alisema katika kipindi cha Januari hadi Julai, mwaka jana, vimetokea vifo 1,139, wakati Januari hadi Julai 2019 vimetokea vifo 896 na jeshi hilo limefanikiwa kupunguza vifo 243 sawa na asilimia 21.

Kwa upande wa majeruhi, alisema kuanzia Januari hadi Julai, wakati Januari hadi Julai mwaka huu, walikuwa 1,759, wamefanikiwa kupunguza majeruhi 619 sawa na asilimia 26.

Alisema kwa upande wa ajali za pikipiki kuanzia Januari hadi Julai, mwaka jana majeruhi walikuwa 556, huku Januari hadi Julai, mwaka huu imefikia 388 na kufanikiwa kupunguza majeruhi 619 sawa na asilimia 26.

Pia alisema vifo vitokanavyo na pikipiki kuanzia Januari hadi Julai, 2018  ni 233 na Januari hadi Julai, mwaka huu  ni 208 na kufanikiwa kupunguza vifo  25 ambavyo ni sawa na asilimia 11.

Majeruhi Januari hadi Julai mwaka jana ni 450 wakati mwaka huu ni 329.

Vile vile, alisema wameanza operesheni ya kukamata madereva ambao hawasimami katika vivuko vya watembea kwa miguu, wakiwamo wanaokwepa kulipa madeni ya faini ndani ya siku saba baada ya kufanya kosa barabarani.

Kamanda Musilim alisema wataendelea kusimamia suala la uwapo wa madereva wawili katika magari yanayokwenda safari za mbali, ikiwamo kuweka askari katika vituo.

Pia alisema wamebaini madereva wa magari makubwa kuchomoa breki za nyuma ambazo zinasababisha gari kuwashinda katika mteremko.

Habari Kubwa