Hongera TGNP ya robo karne iliyobeba vikokotoo vya Beij

06Sep 2019
Yasmine Protace
DAR ES SALAAM
Nipashe
Hongera TGNP ya robo karne iliyobeba vikokotoo vya Beij

MIAKA 25 si mchezo. Kwa binadamu, ni mtu mzima tena ametimia kisawasawa, kwa haki zote za ki- utu uzima. Ikihesabiwa miaka inatisha. Ni simulizi ya robo karne hivi. Kama uliganishi na umri wa mnyama simba, basi ni ‘mbabu’ kama siyo ‘mbibi.’

Nikirudi katika kinachonituma kuandika hivi sasa, nikiwa mshabiki na mtetezi wa jinsia, ni umri sawa na yanayotendwa na chombo chetu kinachotetea pande zote za jinsia, ikitaka kushuhudia haki.

Lakini, mzizi wa mwanzo wa chombo hicho ninachoanza kukieleza kwa mafumbo, asasi ya TGNP Mtandao, ni utetezi wa haki za kinamama, katika mustakabali mpana na mafanikio iliyoyapata, kwani ni ya kutupa furaha. Laiti ningekuwa jukwaani, ningehamasisha watu kuitikia ‘oyee’ na kuomba vigelegele kwa kinamama.

Ni rasmi imetimu miaka 25 tangu TGNP Mtandao kuanzishwa na harakati zake za kumkomboa mwanamke kitaifa. Iko katika hatua ya umri robo karne.

Katika kutimiza miaka hiyo, limeandaliwa tamasha la jinsia ambalo litakutanisha watu zaidi ya 1m 500 kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.

Kuwapo tamasha hilo, naimani kutasaidia washiriki kufahamu mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanywa na asasi yetu TGNP Mtandao, sisi wanahabari kina dada kwa kina kaka, ni wadau wake hasa.

Mbali na TGNP Mtandao, kuandaa tamasha hilo, pia ni siku ambayo Beijing inatimiza miaka 25 toka watoke kupigania harakati za kumkomboa mwanamke kutoka alipokuwa hadi sasa alikofikia.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi anasema katika kutimiza miaka hiyo,wameandaa tamasha la jinsia, litakalojumuisha zaidi ya washiriki 1500 na la siku nne, kati ya Septemba 23 hadi 27.

Anasema kuandaliwa tamasha hilo, kutatoa fursa mbalimbali kwa washiriki kunufaika nazo, kutokana na kubadilishana mawazo yao.

Lilian anasema, katika tamasha hilo maudhui ya mjadala wa Beijing yatajadiliwa na kutoa picha ya tangu walipofanya kikao hicho Beijing na kuzungumzia mafanikio tangu walipotoka jijini Beijing.

Anasema, ni historia ya harakati za ukombozi kwa wanawake, kuwa azimio la mkakati wa Beijing, katika mpango kazi wa harakati za ukombozi kuwalinda wanawake.

Mkurugenzi huyo wa TGNP Mtandao, anasema asasi hiyo za kiraia ilianzishwa ili kutetea haki za wanawake, mzizi wake ni walioratibu safari hiyo kati ya mwaka 1991 hadi 1995. Kuanzishwa kwake rasmi ni mwaka 1993.

Lilian anasema, watu wengi hawajui uhalisia wa dhana ya jinsia na kuona kuwa ni neno linalomhusu mwanamke pekee yake.

Kwa mujibu wa Lilian, baada ya kuanzishwa ikiwa na idara moja pekee, idara ya pili ilibuniwa baada ya kugundua upana na haja ya jamii kufahamu masula yanayohusu jinsia.

Anasema ni idara iliyokuwa inatoa uelewa mpana kwa masuala mbalimbali ya kiserikali na asasi za kiraia na idara ya tatu ilisaidia masuala ya ushawishi usuluhishi na utetezi, kuleta mabadiliko kwa katika masuala ya sera, baada ya kubaini uhaba katika masuala hayo ya kijinsia.

Habari Kubwa