Mimea ya maajabu inayokula wadudu yapandwa Uingereza

10Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mimea ya maajabu inayokula wadudu yapandwa Uingereza

MIMEA inayokula nyama iliyo hatarini kuangamia (Watch a carnivorous plant devouring an insect), imeanza kupandwa tena kwenye maeneo kadhaa ya Uingereza katika jaribio la kupunguza kuangamia kwake.

Wadudu huvutiwa na majani ya mmea huo.

Wataalam wa mimea wanasema kwamba mimea hiyo iliyo na umbo la kuvutia, imetoweka katika sehemu nyingi kutokana na uhaba wa maeneo yenye ardhi zenye unyevu.

Ikiwa na mikono inayoshika na kula wadudu, mimea hiyo ni miongoni mwa makumi ya mimea inayokula nyama nchini Uingereza.

Charles Darwin alifurahishwa sana na aina ya mimea hiyo, na hivyo basi kukusanya picha na vipimo katika kitabu chake kwa jina Insectivorous Plants, kilichochapishwa 1876.

Anasema kwamba aliupendelea sana mmea kwa jina la Drosera, unaofahamika kama Dawy kwa lugha ya Latin, ikilinganishwa na kitovu cha aina zote duniani.

Ni aina iliyo nadra kupatikana kulingana na Joshua Styles kutoka Chuo Kikuu cha Cheshire, ambaye alianzisha hisani yake ya hifadhi kwa jina North West Rare Plant Initiative, kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

Nchini Uingereza, mmea huo umeorodheshwa kama ulioangamia na hupatikana chini ya maeneo 20.

“Hivyo basi kutopatikana kwake na hali yake kulinishawishi kutaka kuupanda tena,” anasema Joshua Styles.

JE MMEA HUO UNAPATIKANA WAPI?

Ulikuwa ukipatikana kwa wingi nchini Uingereza na ulianza kuangamia katika karne iliyopita.

Mabadiliko ya matumizi ya ardhi yamesababisha kukauka kwake katika maeneo yenye ardhi zilizo na unyevu.

Hata hivyo, Styles amefanikiwa kupanda mmea huo kutokana na majani yaliyokatwa na yaliyotoka katika mimea michache iliyosalia, ambayo imeweza kustahimili mazingira magumu kwenye eneo la Cumbria.

Alizindua mimea aina 10 katika eneo la Rsley Moss karibu na Warrington, akishirikiana na wakfu wa Chesser na ule wa wanyama pori wa Lancashire.

Mmea huo unaokula nyama umestahimili katika mazingira hayo na kuanza kuzaana.

“Kila mwaka wakati unapotoa maua, unatoa makumi ya maelfu ya mbegu ndogo ndogo zinazofanana na vumbi,” anasema.

Unapopanda 10 haionekani kama ni mingi, bali idadi ya mbegu zinazotolewa…ninatumaini kupata mbegu nyingi mwaka ujao,” anasema.

MMEA WA SUNDEW

(DROSERA ANGLICA)

Kawaida mimea hujipatia chakula kutoka kwenye mchanga kupitia mizizi yake, lakini mimea inayokula nyama imepiga hatua ya kula protini za wanyama.

Mmojawapo ya mimea hiyo ni wa Sundew ambao una ‘mikono’ mingi midogo midogo inayotoa maji yenye harufu tamu, ambayo huwavutia wadudu.

Mikono hiyo midogo baadaye huwashika wadudu hao na kuwakamua ndani ya majimaji hayo yanayonata.

Enzymes za mwilini hujitokeza polepole na kuwavunja wadudu hao kuwa chakula chenye virutubishi.

Mtunzaji mdogo kabisa wa bustani alivutiwa na utaalamu wa mimea akiwa na umri wa miaka saba, na amekuwa akisoma mimea tangu hapo.

Anasema ni muhimu kuhifadhi mimea ya kula nyama kwa faida yao kwa mazingira na viumbe hai, na kwa faida ya baadaye, kama vile chanzo kinachoweza kutengeneza dawa mpya.

Habari Kubwa