Twiga Stars waililia serikali

19Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Twiga Stars waililia serikali

CHAMA cha Soka cha Wanawake Tanzania (TWFA), kimeiomba serikali na wadau mbalimbali kuongeza nguvu katika kuwekeza kwenye soka la wanawake ili nchi iweze kupata mafanikio zaidi, imeelezwa.

Twiga Stars.

Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa TWFA, Amina Karuma, katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya wanawake ya umri chini ya miaka 20 (Tanzanite), ambao walitwaa ubingwa wa mashindano ya COSAFA mwezi uliopita.

Karuma alisema timu za wanawake zimekuwa zikifanya vema katika mashindano mbalimbali, lakini wanaamini wakiendelea kupewa nguvu, watafika mbali.

"Kama serikali na wadau, wakiwekeza japo robo ya nguvu wanayotumia kwa wanaume, nina hakika tutacheza Kombe la Dunia la Wanawake," alisema Karuma.

Kwa sasa kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), kinajiandaa kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika Novemba mwaka huu hapa nchini.

Habari Kubwa