Mamilioni waliohamia mbadala sigara kielektroniki, madhara kwao palep

19Sep 2019
Michael Eneza
DAR ES SALAAM
Nipashe
Mamilioni waliohamia mbadala sigara kielektroniki, madhara kwao palep
  • Misiba tata yaibua maswali yanayoelea
  • Bangi na tumbaku zajitokeza kivingine
  • Wataalamu wakali wakihoji ya Trump
  • “…Walitumia sigara mtandao zenye ‘nicotine’ (kiungo cha kawaida cha sigara)…baadhi wanasema walitumia sigara mtandao yenye kemikali inayoitwa THC ambayo ina ‘marijuana’ (bangi laini zinazouzwa Marekani) kuweza kuwapatia hisia za ulevi au ‘nishai’…. hadi w

KUNA jipya nchini Marekani ambalo sasa ni ‘habari ya mjini’ kuhusu kuongezeka vifo vya vijana wanaoshiriki mchezo wa ulevi mpya kimtandao.

Wahusika wakivuta sigara za kieketroniki.

Suala ni kwamba, mtu anazoea sigara yenye aina fulani ya unyevu. Hiyo inaitwa sigara ya kielektronikia au maarufu ‘e –cigarette’

Hicho ni kifaa mithili ya sigara iliyowekewa mvuke na mvutaji anatumia kama vile sigara ya kawaida kwa mbwembwe na burudani nyinginezo ya uvutaji, lakini kamwe haina uhusiano na tumbaku.

Tendo la kutumia sigara hiyo na kupumua ‘moshi wa mvuke unamfanya mvutaji afaidi, kana kwamba anavuta na sigara hizo ziko za aina nyingi, mithili ya sigara za kawaida na kiko, utengenezaji wake ukipitia mitindo na awamu mbalimbali kuligana na wakati.

Ni hali iliyochangia kupatiwa jina ‘vaping’ kwa maana ya kutumia kitu chenye mvuke (vapor). Bado inaelekea ni nchini Marekani, ulevi huo ndiko ulikoshika kasi zaidi na vifo tayari vimesharipotiwa vingi.

WATAALAMU WABISHA

Bado kuna mjadala wa kitaalamu kama sigara hizo zisizo na vimelea vya nikotini, ambavyo vinapatikana katika tumbaku na vina athari kiafya au la.

Jambo pekee lililo bayana ni kwamba hadi sasa inajulikana pamoja na manufaa yake kumnusuru mvutaji kumuweka mbali na athari za kuacha sigara, hailinganishwi na kuacha kabisa.

Shaka nyingine inayoanikwa kitaalamu ni kwamba, vijana wanaotumia sigara hiyo bandia, wako katika nafasi kubwa ya kutumbukia katika matumizi ya sigara ya kawaida.

Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini Marekani (UF DAS), iko katika msimamo wake kwamba mbadala huo wa nikotini (tumbaku) ambayo ni ‘e- cigarette’ ni salama zaidi.

MAONI WATAALAMU

Wakati baadhi ya wataalamu wa afya wanataka sigara hizo na kupatikana kwake katika mtandao kupigwe marufuku kuna wanaosema jitihada kama hiyo ya kueneza sigara za kielektroniki itazaa madhara zaidi, badala ya ahueni inayotarajiwa. 

Jarida linaloheshimika la uchumi la kila wiki nchini Uingereza, The Economist lina maoni ya wachumi Marekani, wanakosoa sera za utawala wa Rais Donald Trump, kupunguza hatua au hitaji la kuthibitishwa kwa bidhaa, kabla ya kuwekwa  sokoni.

Dai ni kwamba, ingebidi sigara hizo zikaguliwe kwa kina na Mamlaka ya Chakula na Dawa ipate kibali kabla ya kuingizwa sokoni kuuziwa mteja mmoja mmoja.

Hiyo ni baada ya watu sita kuripotiwa kufariki kutokana na kuvuta sigara oevu za kimtandao. Maofisa wa afya katika majimbo tofauti ya Marekani, walianza kutoa sauti zao kuwa ‘ku-vepa’kukomeshwe.

VIFO VYAMEA  

Hadi wiki moja iliyopita, inaripotiwa mbali na vifo vya 12, zaidi ya watu 450 walishapata madhara makubwa katika mapafu. Baadhi ya wataalamu walikuwa na shaka kuhusu wakiegemea wazo la ulazima wa kupigwa marufuku bidhaa hiyo inayomea.

Moja ya sababu kubwa ni mtandao mpana wa wavutaji sigara oevu sasa wamefikia wastani wa milioni 11 hivi. Taasisi ya Udhibiti wa Maradhi na Chama cha Madaktari Marekani, kwa pamoja walitoa mwito wavuta ‘vepa’ hao milioni 11 kuacha, wakiwaambia ni hatari kuliko kuvuta

 Utawala wa Rais Trump, ulitamka Septemba 11 iliyopita kuwa unataka kupiga marufuku kimiminika hicho ambacho si cha tumbaku, lakini wapo ambao kupitia vyombo vya habari hawaridhishwi na hoja hiyo, wakiwa kinyume katika wanachokiita ‘kutetea uhuru.’

Mtaalamu mmoja akichangia uchambuzi katika jarida la Uingereza, anasema dondoo muhimu za suala hilo zinaachwa pembeni kwani inapotokea hatari kwa afya watu wengi, mihemko inachukua nafasi ya uchambuzi wa kina, kuangalia hali halisi ilivyo.

 Anatoa tahadhari kuwa bado utafiti wa ziada unahitajika, kwani ushahidi uliopo unaonyesha kuwa vifo vinavyohusishwa na ‘kuvepa’ nchini Marekani, havikutokana na bidhaa zilizouzwa dukani, ila kutokana na vitu vilivyotengenezwa bila umakini na kuuzwa barabarani.

Msomi huyo katika hoja yake, anadai vifo vitano kati ya sita vilivyohusishwa na kimiminika kilichotumika kilinunuliwa kienyeji, wakati kifo kimoja kilitokana na kimiminika kilichonunuliwa katika duka lililosajiliwa la bidhaa za jamii ya tumbaku (cannabis), jimboni Oregon.

Anasema, kuna nadharia inayoelezea athari mbaya za  kimiminika husika kilichanganywa na Vitamini E, akifafanua ni mafuta na hayatakiwi kabisa kuingia katika mapafu. Anasema mtu anayevuta mafuta yanamletea madhara kama hayo ya ‘wavepaji.’

Taasisi ya Kuzuia Maradhi, inasisitiza katika taarifa kuwa yake kuwa bidhaa za kuokotwa barabarani ndizo zinazua hatari kubwa, siyo kwa ‘wavepaji’ peke yao, hata wanunuzi wa ‘bangi’ za mitaani katika maduka yasiyosajiliwa.

Hivyo, watengenezaji bidhaa za ‘kuvepa’ wanatakiwa kuboresha bidhaa na mahitaji yao yamtandao, yenye ladha, katika juhudi za kukabiliana na magonjwa ya mapafu yanayohusishwa na ‘kuvepa.’

Zaidi ya majimbo 25 nchini Marekani kati ya takriban 50 wameeleza kushtushwa na hali ya magonjwa ya mapafu yanayohusishwa na ‘kuvepa’ kudhihirisha kuwa tatizo ni kubwa na linaenea.

Jarida la Uingereza lilitofautiana na taasisi hiyo ya Marekani katika mapendekezo yake, likitahadharisha  kuwa watu wanaojali afya zao wasiguse kabisa sigara ‘oevu’ za mtandaoni, bali watafute ushauri wa daktari wanapojitahidi kuacha kuvuta sigara za kawaida.

Taasisi hiyo inasisitiza kuwa sigara za mtandaoni zisitumiwe na vijana wadogo wanaofikia umri wa kuwa wakubwa kisheria, mama wajawazito na watu wazima ambao hawatumii bidhaa za tumbaku.

Asasi hizo zinawaasa hasa vijana kuwa mtumiaji sigara oevu za mtandaoni, achunge afya yake kwa kuangalia dalili za magonjwa, kwa mfano kukohoa, kukosa hewa, maumivu kifuani na ikibidi atafute ushauri haraka kutoka kwa wataalamu wa afya.

Idadi ya wenye matatizo makubwa ya kupumua sasa ilishafikia 2,156 katika majimbo 25 na kuanzia mwisho wa Juni iliyopita, wengi wamelazwa hospitalini wakiwa na matatizo ya mapafu yanayoonekana kuwa sugu.

Hao ni wanaoelezwa kuwa wanahitaji msaada wa mashine wapumue na kuangaliwa kwa karibu hali zao, hivyo sifa zao ni kuwa katika chumba cha uangalizi maalumu hospitalini (ICU).

VIFO JE?

Mishtuko ilienea baada ya kuwapo taarifa  za mwanamke mwenye umri miaka 30 hivi karibuni alikufa jimboni Illinois, alipoanza ‘kuvepa.’

Maofisa wa afya wanaeleza kusubiri vielelezo kuhusu sumu mwilini mwake na uchunguzi wa aina tofauti, kutambua kilichomsibu hadi kifo.

Baadhi ya waathirika wanasema, walitumia sigara mtandao yenye kemikali inayoitwa THC ambayo ina ‘marijuana’ (bangi laini zinazouzwa Marekani) kuweza kuwapatia hisia za ulevi au ‘nishai.’

Baadhi ya madaktari walifuatilia matukio ya magonjwa hayo, wanasema kuwa mafuta ya bangi ambayo yamegandishwa kuwa na unyevu kujazwa kwa kifaa katika ‘flash’ yanaweza kusababisha kuungua mapafu.

Waathirika wengine waliohojiwa wanasema, walitumia sigara mtandao zenye ‘nicotine’ (kiungo cha kawaida cha sigara) na katika matukio mengi zaidi, waathirika walielezea kuongezeka polepole viashiria vya athari hasi.

Hapo ina maana ya kupumua kwa tabu na maumivu kifuani kabla ya kulazwa hospitalini, kupata chanzo cha pamoja, bado ilikuwa ngumu.

Baadhi ya wataalamu walikuwa wanajiuliza kama kuna magonjwa tofauti mwenye viashiria vinavyofanana, huku mtaalamu wa The Economist aking’ang’ania kuwa ufahamu uliopo kuhusu kemikali za sigara mtandao bado ni mdogo licha ya kuwa hazina ‘lami’ (mgando) na visabishi vingine vya saratani katika bidhaa jadi za tumbaku.

Ila mtaalamu anakubali ‘kuvepa’ kuna changamoto za wazi, kwani ili kuweza kupulizwa nikotini ya kawaida au THC, lazima mtu ichanganywe na vimimino vinayoyeyusha na hivyo ‘kuopoa’ kinachotakiwa kuvuta, au kilevi kinachotakiwa.

Kiongozi wa zamani wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Dk. Scott Gottlieb, anasema baadhi ya kemikali hatari zinahusiana na vimelea vya bangi au THC.

‘Inaelekea ni kitu kipya kilichoingiwa sokoni na kiwanda kisichosajiliwa, kisabibishi ladha kipya au njia mpya ya kuyeyusha THC ndiyo inaleta maumivu haya.’ Mamlaka hiyo ilisema inafanya mchanganuo wa sampuli 80 za waathirika.

VINASABA VYABOMOKA

Katika hatua nyingine wataalamu wa Kimarekani wamefanya utafiti na kugundua kwamba matumizi ya sigara za elektroniki yanakaribisha janga la kubomoa vinasaba vya mtumiaji na kukaribisha maradhi, ikiwamo moyo, mapafu na kansa.

Inaelezwa, uvutaji wa sigara hizo unaleta hatari ya tabu kiafya zaidi katika maeneo kama mapafu na utumbo, kuliko hata kwa namna ilivyo, kwa anayetumia sigara za kawaida.

Timu ya madaktari mabingwa wa Marekani, ikiongozwa na daktari Moon-shong Tang, kutoka Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha New York, anasema ni aina ya sigara inayoweka hatarini zaidi afya ya mtumiaji.

Kupitia ripoti yao inayopatikana katika Jarida la   kitaaluma la kisayansi, wanasema uvutaji sigara hiyo ya kielektroniki inasababisha zaidi kansa ya utumbo na magonjwa ya moyo.

Madaktari hao walipozamisha ujuzi wao kulinganisha athari za mtumiaji sigara kielektroniki na namna ilivyo karibu na kansa, katika namna ileile alivyo mtumiaji sigara za kawaida, afya inadhurika katika namna inayofanana.

Watafiti wanasema, wakati hali ni hiyo, utumiaji wa sigara hizo uko juu kwa vijana wadogo wanaojihisi wako mbali na kudhurika, kutokana uhalisia wa umri walio nao

“Pia, ni muhimu kufahamu kwamba watumiaji wa sigara za kielektroniki wanaichukulia kama tabia na si mbadala kuacha sigara za tumbaku, wako katika mtazamo wa jumla kwamba ‘e –cigarette’ ni salama,” wanaeleza wasomi hao.

Wakati ripoti ya kiserikali ikionyesha kuwapo wavutaji milioni 11, wasomi hao kupitia utafiti wanabashiri wapo milioni 18 nchini Marekani na kati yao asilimia 16, (million 28.8) ni wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Habari Kubwa