Uchafu tabia za watoto tunaendaje nayo Kivule?

11Oct 2019
Yasmine Protace
Nipashe
Uchafu tabia za watoto tunaendaje nayo Kivule?

UKATILI wa kijinsia umekuwa ukipingwa katika maeneo mbalimbali nchini, kutokana na kukiuka haki za mtu anayefanyiwa ukatili huo.

Katika kupambana na matukio hayo, serikali imeweka madawati katika vituo vya afya, pale anapofanyiwa mtu matendo hayo, anapaswa kupatiwa huduma muhimu za kimatibabu.

Ni jambo ambalo kero yake sasa inahusu sehemu kubwa ya umma. Kuna asasi mbalimbali zimekuwa zikilaani matukio hayo na kuamua kutoa elimu kwab jamii jinsi ya kujikinga nayo.

Pamoja na jitihada hizo za serikali, bado kuna baadhi ya jamii nao watoto wanaofanyiwa matukio hayo na wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa polisi wakikumbatia dhana ya ‘kumalizana wenyewe’ huku wakijua wanamuumiza aliyetendewa kitu hicho.

Diwani wa Kata ya Kivule jijini Dar es Salaam, Willson Mollel, anakiri kupata taarifa chafu katika kata yake na kwamba wanachukua hatua ya kutoa elimu mbalimbali na akisema kuna hatua.

Mollel anasema katika moja ya shule zilizoko katika kata yake, mwanafunzi wa sekondari alituhumiwa

dhidi ya vitendo hivyo kwa mtoto wa shule ya msingi wa kata nyingine.

Cha kushangaza, inadaiwa mwanafunzi wa shule ya msingi aliyetendewa amehamishiwa mkoa tofauti na anaendelea na masomo na aliyeathiriwa, kwa sasa hafiki shule, jitihada za kumtafuta zikiendelea.

Inadaiwa kijana anayetuhumiwa kutenda kosa haishi na wazazi wake wawili na simu ya mzazi wake inaelezwa haipatikani kwa sasa.

Malalamiko ni kwamba, mtoto huyo kuhamishwa na kutoweka ni kitendo cha makisa, kwa sababu ni kumpotezea haki yake.

Kwa nini hivyo? Malalamiko yako ikiwamo kutoka kwa Diwani Miolle, akilalamikia tabia mbaya kwa vijana wadogo, ikiwamo uvutaji bangi.

Diwano Mollel anasema kuna wakati uongozi wa polisi kituo cha Stakishari Ukonga, uliwaita madiwani wote wa kata zinazozunguka eneo hilo, pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa, kujadili jinsi ya kutokomeza uvutaji bangi katika maneo yao.

Mwalimu wa shule ya sekondari iliyopo katika Kata ya Kivule, anasema ‘vijiwe’ vya bangi ni vingi na vinachangia kuwaharibu wanafunzi.

Anasema, pia kuna baadhi ya majengo ambayo hayajakamilika, kwamba ni tatizo linalokaribisha uvunjaji sheria kwa watoto.

Mwalimu anakiri kulijua tukio chafu lililowakuta wanafunzi wao, ikiwa matunda ya kazi ya klabu za wanafunzi inayoratibiwa na jumuiya anayoitaja kwa kifupi, GDSS, kwamba ilitoa taarifa ya mwanafunzi kulawitiwa na mwanafunzi mwenzake.

Smulizi yake ni kwamba, baada taarifa hiyo,

walimhoji mwanafunzi huyo na akakubali kuwa aliwavutisha bangi watoto watano wa shule ya msingi na ndipo alipowalawiti kwa zamu.

Anasema pamoja na mwanafunzi huyo kukiri, alipotea shule na mpaka sasa hajaonekana.

Kwa mujibu wa mwanaharakati Selemani Bishagazi, matukio ya ulawiti mengi yanatokana na mfumo wa maisha uliopo.

Anataja mojawapo ni wavulana kulala chumba kimoja na wengine kulala na ndugu zao wa jinsia moja.

Habari Kubwa