Stars kamili yawasili Kigali

12Oct 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Stars kamili yawasili Kigali

KIKOSI cha Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars), kiliwasili salama jijini Kigali, Rwanda jana asubuhi, tayari kuwakabili wenyeji katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa Jumatatu nchini humo.

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Suleiman Matola, alisema jana kuwa uamuzi wa kwenda mapema Kigali, umetokana na kuhitaji nafasi zaidi ya kukiimarisha kikosi hicho katika eneo tulivu zaidi.

"Tumeshafika Rwanda, tuliamua kuja huku (Kigali) mapema kwa sababu zetu za kiufundi, kuna programu ambazo mwalimu alitaka tuzifanye tukiwa nje ya nyumbani, pia itawapa nafasi wachezaji kupumzika vema na kusubiri mchezo," alisema Matola.

Stars inatarajia kutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi ya kuwavaa Sudan katika mechi ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayochezwa Oktoba 18 mwaka huu mjini Omdurman.

Habari Kubwa