Babu Seya, Papii Kocha jukwaani

18Oct 2019
Steven William
MUHEZA
Nipashe
Babu Seya, Papii Kocha jukwaani

MWANAMUZIKI Papii Kocha "Mtoto wa Mfalme" kwa kushirikiana na mkongwe wa muziki nchini, Nguza Viking maarufu, Babu Seya wanatarajiwa kushusha burudani ya kukata na shoka wilayani Muheza na Korogwe mkoani Tanga baadaye mwezi huu.

Shoo hizo mbili zilizoandaliwa na   mfanyabiashara maarufu wilayani Muheza, Teddy Elieti kwa lengo la kuwaburudisha wakazi wa wilaya hizo mbili, zitaanzia Muheza Oktoba 25, mwaka huu kabla ya kesho yake wanamuziki hao kwenda kufunga kazi Korogwe.

Elieti alimwambia mwandishi wetu kuwa Nguva Viking maarufu Babu Seya kwa kushirikiana na mwanawe, Papii Kocha wameahidi kushusha burudani ya nguvu na kuwataka wakazi wa Muheza, Korogwe na Tanga kwa ujumla kujitokeza kwa wingi na wasingoje kuhadithiwa.

Alisema mbali na tungo zao zilizozoeleka, pia wanamuziki hao watashusha nyimbo za manguli wa kali zikiwamo muondoko wa rhumba na nyinginezo kali.

Habari Kubwa