Milioni 1.4 zakusanywa kusaidia elimu

21Oct 2019
Daniel Sabuni
Kilimanjaro
Nipashe
Milioni 1.4 zakusanywa kusaidia elimu

Shirika la Compassion International likishirikiana na wadau kutoka Uholanzi, wamechangisha jumla ya fedha Milion 1.4 kupitia michezo ya hisani inayofahamika kama Muskathlon kwa lengo la kusaidia watoto wa kitanzania hasa katika suala la elimu.

Baadhi ya wageni waliochangisha kiasi cha Dola mil 1.4 kutoka uholanzi wakifurahia jambo wakati wa mapokezi kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Compassion Inetrnation baada ya kuwasili uwanja wa ndegewa Kilimanjaro. Picha na Dniel Sabuni

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mapokezi ya wageni 158 kutoka nchini Uholanzi, Mkurugenzi wa Shirika la Compassion  International, Mary Lema amesema fedha hizo zimetolewa na wadau wenye mapenzi mema kwa ajili ya kusaidia watoto na jamii ili kujikwamua na suala la umasikini.

Lema amesema fedha hizo zitatumika kwa watoto kupitia taasisi zinazofanya kazi na Shirika la Compassion hasa makanisa ya kiinjili kwa kuboresha miradi ya maji, elimu na mahitaji mengine yanayolenga kumsaidia mtoto ili kuepuka na wimbi la umasikini na kuleta maendeleo.

Aidha, amesema wageni wote watapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Arusha, ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Tarangire ili kuchangia pato la Taifa kupitia fedha za kigeni. Hivyo itasaidia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Naye Mdau kutoka Nchini Uholanzi, Wouter De Vos Muskathlon, amesema kwa niaba ya wachangishaji watahakikisha zoezi hilo la uchangishaji linakuwa ili kuongeza fedha za kumsaidia mtoto wa kitanzania.

Mpaka sasa Compassion Iternational inashirikiana na makanisa zaidi ya 470 katika Mikoa 19 na zaidi ya Halmashauri 80 kwa Tanzania Bara.

Habari Kubwa