Wananchi watakiwa kondokana na dhana potofu juu ya chanjo

21Oct 2019
Dotto Lameck
Singida
Nipashe
Wananchi watakiwa kondokana na dhana potofu juu ya chanjo

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo, amewapongeza wazazi pamoja na walezi kwa kujitokeza kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo.

Amezungumza hayo katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya kuzuia magonjwa aina ya surua, rubella na polio iliyofanyika kwenye kituo cha Afya cha Ikungi, huku akitoa taarifa fupi ya maandalizi ya chanjo ya magonjwa hayo na kuwasihi kuwa chanjo ni muhimu kwa kuwa inaweza kusababisha ulemavu, upofu pamija na vifo kwa watoto

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Huduma za jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Abeli Richard Sui, ameishauri jamii kuondokana na mila potofu za kuamini kuwa endapo motto akipatiwa chanjo ya ugonjwa wa Surua, Rubela na Polio kuna uwezekano wa kupata madhara kwa siku za baadae.

Amesisitia kuwa ni wakati muafaka kwa wataalamu wa Afya kwa kushirikiana na wanasiasa kwenda kuwahamasisha wananchi kwa kuwapatia elimu sahihi ili waweze kuondokana na dhana hiyo potofu. 

“Yapo mambo katika jamii ambayo kwa umoja wetu tunaweza kuyaondoa kama tukienda kuielimisha jamii ili ifahamu umuhimu wa hiki kwa sababu baadhi ya jamii wanaona mtoto akichanjwa pengine anaweza akapata madhara baadae” Amesema Sui.

Naye muwakilishi wa Wizara ya Afya, Honest Nyaki amewaomba wazazi na walezi wenye watoto ambao wanasifa za kupatiwa chanjo ya magonjwa hayo kuwapeleka watoto hao kupatiwa chanjo.

Aidha, Nyaki amebainisha kuwa mazazi yeyote Yule ambayehataweza kumpeleka mtoto wake kupatiwa chanjo atahesabika kufanya kitendo cha hujuma kwa motto.