DAWASA yakesha kutengeneza bomba ili kurejesha maji

22Oct 2019
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
DAWASA yakesha kutengeneza bomba ili kurejesha maji

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imejikuta ikikekesha usiku na mchana katika kuhakikisha inarejesha maji kwa baadhi ya wakazi wa maeneo ya jiji la Der es Salaam, kutokana na kukatika kwa bomba kuu la inchi 54 linalosafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Meneja usambazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Eng. Tyson Mkindi amesema wamekuwa hapo kutokana na maji yalikuwa yamekatika  kwa siku tatu mfululizo.

"Jitihada za kuwarejeshea maji wakazi wa maeneo mbalimbali zinaendela na zipo katika hatua za mwisho ingawa  kazi ya kurekebisha bomba hilo imechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kufuatia kuwepo kwa maji mengi katika mto Rufiji". Amesema Eng. Mkindi.

Mkindi amesema kuwa, chanzo cha kukatika kwa bomba hilo kuu na kushindwa kusafirisha maji kutoka mtambo wa Ruvu chini inasababishwa na uchimbaji holela wa mchanga katika mto Rufiji na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.

Hata hivyo Dawasa imechukua hatua ya dharura kwa kuchukua maji kutoka katika bomba jipya la inchi 72 na kuyaingiza katika bomba la zamani la zege ambalo litazibwa kabla na baada ya mto ili kuruhusu wananchi walio kosa maji kupata huduma hiyo kama awali. Amesema Eng. Mkindi

Aidha,Mkindi ametaja maeneo yaliyoathirika na uharibifu wa bomba hilo ni Kerege, Mapinga, Kiharaka, Kiembeni, Mingo, Kilemela, Kimele, Vikawe, na Amani. Hivyo amewasihi wavute subra.

Habari Kubwa