Kibiti wanapojivunia mageuzi ‘umwinyi’ basi, mapato juu

14Nov 2019
Yasmine Protace
Nipashe
Kibiti wanapojivunia mageuzi ‘umwinyi’ basi, mapato juu

MARA zote mapato yanaposimamiwa katika sehemu yoyote, iwe binfasi ya kiserikali, kuna mafanikio lazima kushuhudiwa.

Na mapato hayo yanapopatikana na katumika vizuri, basi ni dhahiri yanatoa matokeo chanya, kwani yanasaidia uboreshaji kwa namna nyingi.

Hiyo ndio maana kuna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambayo mbali na kukusanya mapato ya ushuru na kodi za kiserikali, pia mapato mengineyo, kwani ni wakala mkuu wa serikali katika jambo hilo.

Tumekuwa tukisikia na kujionea serikali inavyosema kuwa inaboresha mambo na majukumu yake katika eneo fulani. Nyuma ya pazia ni matokeo ya usimamizi mzuri wa mapato ya kiserikali na kodi. Rais Dk. John Magufuli, mchana kwa asubuhi huwa ni mhubiri wa hilo. Anaeleza mafanikio ya serikali yake kufanikisha mengi, tena mazito. Yote ni zao la usimamizi wa mapato ya umma.

Dhana ya mapato hata kuangukia ngazi ya mtu binfasi, asipokuwa makini binafsi na kibishara, katika kujisimamia anaweza asifike mbali katika masuala ya kimaendeleo.

Atabaki kuwa shuhuda wa kuwahi kushika fedha au kuwa karibu nazo bila ya mafanikio. Hivyo, inatakiwa mtu ajifunze suala la kusimamia mapato yake aweze kunufaika nayo.

Yapo mashirika ambayo yamekuwa yakifundisha jamii juu ya kusimamia mapato. Lengo ni kuiwezesha jamii imudu kujitambua katika suala zima la usimamizi wa mapato.

Kama mapato yasiposimamiwa kikamilifu, ukiuwaji katika eneo hilo unakuwa wa shida. Mara nyingi mapato yanaposimiwa kikamilifu, kunachangia kuwapo maendeleo mazuri katika eneo hilo. Ndio tunda maendeleo linapozaliwa.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibiti mkoani Pwani, Khatibu Chaulembo, alisema wamejipanga kimkakati kuviinua vyanzo vyoye vya mapato.

Anasema, kwa miaka ya nyuma hawakuwa wanafanya vizuri katika suala zima la ukusanyaji mapato, akitamka:" Tumepata Mkurugenzi (Mtendaji) mpya, Mohamed Mavula, ambaye ana uwezo katika kusimamia ukusanyaji wa mapato.”

Anaongeza kwamba, halmashauri ina vyanzo mbalimbali vya mapato, ikiwamo mapato ya korosho na kiwanda cha samaki aina ya ‘pronzi’ ambacho kilifungwa miaka minane iliyopita na sasa kinatarajiwa kufunguliwa mwezi huu.

Chaulembo anasema awali katika soko la Kibiti hawakukusanya mapato kutokana na adha aliyowaita ‘Mungu mtu’, lakini kwa sasa Mkurugenzi huyo kaondoa ukiritimba uliokuwapo sokoni katika masuala ya ukusanyaji mapato.

Anasema, awali walikukutana na changamoto kubwa pale waliposanya mapato na sasa mkurugenzi mpya amesaidia kuondoa ‘umwinyi’ katika soko hilo, halmashauri ikifunguliwa kukusanya vyake.

Chaulembo anasema mapato ya Kibiti yanatokana na bajeti na kuongeza kuwa malengo ambayo wamejiwekea ni kuongezeka ukusanyaji wa mapato.

Kwa sasa anasema, wameweka vibarua wapya kwa ajili ya kukusanya mapato.

Habari Kubwa