Magufuli ateua mwenyekiti TMA

20Nov 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Magufuli ateua mwenyekiti TMA

Rais John magufuli, amemteua Dk. Burhan Nyenzi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Taarifa ilitoyolewa jana na Kurugenzi na Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilisema Dk. Nyenzi ambaye ameteuliwa kwa kipindi cha pili anatoka Tanzania Bara.

Pia taarifa hiyo ilisema Rais amemteua Dk. Makame Omar makame kutoka Zanzibar kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

Dk. Makame kwa sasa ni Mhadhiri Mwandamizi wa Jiographia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Taarifa hiyo ilimkariri Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, kuwa uteuzi huo ulianza juzi.

Habari Kubwa