Tunapovunja sheria hivi tunategemea nini?

29Nov 2019
Yasmine Protace
Nipashe
Tunapovunja sheria hivi tunategemea nini?

SHERIA inapotungwa mahali popote ni wajibu wa kila mtu kuzifuata. Mtu anayevunja sheria kwa makusudi, anastahili kuchukuliwa hatua.

Kutungwa kwa sheria, lengo lake ni kuwataka watu wazitii, ili zilete manufaa katika eneo husika.

Mara nyingi, kuna makundi katika jamii yamekuwa yakiibuka kukaidi hata maelekezo wanayopewa na ama viongozi au serikali. Inachangia kuangukia uvunjaji wa sheria.

Linalotakiwa ni kwamba, kila mtu anapaswa kufuata sheria, jambo litakapomfanya aanguke katika kuvunjwa sheria za nchi, ambazo kila mtu anapozifuata, hakuna shaka anakuwa mbali na changamoto hizo.

Inawezekana, baadhi yetu hatuzijui kwa undani sheria zilizopo na kusababisha umma kuangukia katika ukiukwaji wake.

Nianze na hili ambalo lipo katika baadhi ya ofisi za serikali na panapopatikana huduma zake, zikiwamo picha zinazoelekeza uvaaji nguo. Mgonjwa anayefuata huduma anapaswa kuvaa nguo zenye maadili, akikiuka unarudishwa nje.

Inawezekana mhusika hakulijua hilo na anapokutana na zuio ndipo linamfungua umevunja sheria za nchi. Hapo inaanza kumpa maswali binafsi, kinachofanya mpaka kuvunja sheria za nchi na baadhi ya sehemu za mjumuiko ni nini?

Kuna nilichokiona hapo katika hospitali kubwa jijini Mwanza, ambako pia kuna chuo cha madaktari na wengine wa fani ya tiba, inashangaza mantiki yake.

Hapo kuna kozi mbalimbali zinazotolewa mahali hapo na kila mwaka kuna wanaofuzu mafunzo hayo ya tiba, huku kukiwapo orodha nyingine kubwa ya wanaochukua nafasi kujiunga na mafunzo.

Katika chuo hicho, ndiko kuna geti linalotumiwa na wanachuo kuingia. Ni mahali kunakopatikana katazo kuingia na nguo zisizofaa kimaadili, ama kwenda kupata matibabu au mahitaji mengineyo ndani ya mazingira hayo. Inawahusu pia wanachuo na wadau wake wote.

Katika geti hilo kunakatazwa kuingia na nguo zisizo na maadili. Nimeshangaza, kuona baadhi ya vijana hawazingatii hilo na wamekuwa wakigombana na walinzi kutokana na kuvaa nguo zisizo na maadili.

Vijana hao wanakatazwa kuingia hospitali kutokana na kuvaa nguo zisizo na maadili, lakini huwa nawashuhudia wanakuwa wakali na wameonewa kurudishwa nje ya geti.

Nilishuhudia malumbano, baadhi ya wanachuo waliporudishwa nje kutokana na nguo walizovaa, walidai nguo walizovaa ‘matilio’ yake inapanda juu na ndio maana zinaonekana fupi.

Mmoja wao, anayefanya kazi katika hospitali hiyo, anasema watoto wengi wanaharibika kutokana na malezi.

Anasema matangazo yapo, lakini wanayapuuzia na kuendelea kuvaa nguo zisizo na maadili.

Habari Kubwa