Ushahidi changamoto mimba za wanafunzi kushamili

05Dec 2019
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Ushahidi changamoto mimba za wanafunzi kushamili

TATIZO la mimba kwa wanafunzi mkoani Shinyanga limetajwa kuendelea kushika kasi kutokana na kesi nyingi kushindwa kufikia hukumu na watuhumiwa kufungwa jela, sababu ya kesi hizo kukosa ushahidi kwa jamii yenyewe kufanya maliziano kimyakimya na kuacha kuhudhulia mahakamani.

Hayo yamebainishwa juzi na Ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo, wakati akiwasilisha taarifa ya mpango mkakati wa Serikali kitaifa wa kupunguza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA, kwenye kikao cha kujadili kutokomeza ukatili huo kilicho andaliwa na shirika la kivulini.

Amesema wanafunzi wa kike kwenye halmashauri hiyo wameendelea kukatishwa masomo yao kwa kupewa ujauzito, kutokana na watuhumiwa kuchochukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo kufungwa jela, na kusababisha jambo hilo kuzoeleka na wanaume kuendelea kuwa tia mimba wakitambua hawatafungwa.

Ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Elizabeth Mweyo akiwasilisha taarifa ya mpango mkakati wa Serikali taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA, na kubainisha taarifa ya robo mwaka kuanzia Julai- Septemba mwaka huu kuna mimba za wanafunzi 18, Sekondari 14, msingi Nne.

“Taarifa ya robo ya mwaka ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuanzia Julai hadi Septemba 2019, wanafunzi 18 wameshapewa ujauzito na kukatishwa masomo yao,14 kutoka shule za Sekondari, Wanne (4) za msingi,”amesema Mweyo.

“Kesi hizi tunapokuwa tukizishughulikia na kuzifikisha mahakamani, nyingi zimekuwa zikiishia njiani kutokana na ushahidi kukosekana, ambapo wahusika wapande zote mbili wamekuwa wakifanya maliziano na kuacha kuhudhulia mahakamani au mhanga kumkana mtuhumiwa na hatimaye kesi kufutwa,” ameongeza.

Ofisa wa dawati la Polisi mkoa wa Shinyanga Victoria Maro, akiwasilisha taarifa ya polisi dawati la jinsia na kubainisha ukatili bado upo ila changamoto wazazi hawataki kutoa ushahidi na hatimaye watuhumiwa kuachiwa huru

Naye mratibu wa (MTAKUWWA) Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale, amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo ya ushahidi, wanaandaa mkakati wa kuwabana wazazi, ambao wamekuwa na tabia ya kumaliza kesi kimya kimya, pamoja na kujenga nyumba salama za kuhifadhi wahanga ili wasirubuniwe kukana watuhumiwa.

Aidha mzee wa kimila Kapaya Sosoma mkazi wa halmshauri ya wilaya ya Shinyanga, amesema tamaduni za kabila la wasukuma hua hawapendi kesi, na diyo maana wanamaliza kesi kimya kimya, pamoja na kuwaambia watuhumiwa wakimbie ili kesi ipate kufutwa mahakamani.

Wadau wa elimu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha kujadili changamoto za ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni na kuzitafutia ufumbuzi

Kwa upande wake Ofisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini Godfley Paschal, wanaotetea haki wa wanawake na watoto, amesema wameendesha kikao hicho ili kujadili changamoto za matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na kuzitafutia ufumbuzi likiwamo suala la mimba za wanafunzi.

Ofisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka Shirika la Kivulini Godfley Paschal, wanaotetea haki wa wanawake na watoto, akiwasilisha mada ya kujadili changamoto za kuendelea kuwepo mimba na wanafunzi na kuzitafutia ufumbuzi

 

Wadau wa elimu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha kujadili changamoto za ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni na kuzitafutia ufumbuzi

Habari Kubwa