DC Mjema ataka walimu shule binfasi kujiunga na chama cha TPTU

11Dec 2019
Kelvin Innocent
Dar es Salaam
Nipashe
DC Mjema ataka walimu shule binfasi kujiunga na chama cha TPTU

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, amewataka walimu wa shule binafsi katika mkoa wa Dar es Salaam, kuhakikisha wanajiunga na Chama cha TPTU kwa dhumuni la kuimarisha ushirikiano wao. 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema

Amesema hayo leo Desemaba 12, 2019 jijini hapa alipokuwa akizungumza katika mkutano na baadhi ya walimu wa shule mbalimbali. Mjema amasema, ni vyema kwa walimu wote wanao fundisha katika shule binafsi kuhakikisha wanajiandikisha kwenye chama hicho kama ilivyokuwa kwa walimu wa shule za serikali ambao ni wanachama ili kujadili mambo binafsi na ya  kimaendeleo.

“Kwa walimu wote wa shule binafsi katika mkoa wa Dar es Salaam wahakikishe wanajiunga na TPTU kwa kuwa hiki ndiyo chama chao kisheria kama ilivyo CWT kwa walimu wenzao wa serikalini,” amesema Mjema.

Hata hivyo, Mjema ametoa kauli ya kuwataka, waajiri na wamiliki wa shule binafsi  kutowafukuza kazi walimu au kuwazuia kujiunga na chama hicho kilichoanzishwa kwa ajili ya walimu wanaofundisha shule binafsi.

“Wamiliki wa shule binafsi za mkoa wa Dar es Salaam, wanatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuwakatisha au kuwafukuza kazi walimu na kuwazuia wasijiunge na TPTU, hivyo wawahakikishie kila shule walimu wao wamejiunga kwenye chama hiki,” amesema Mjema.

Naye Rais wa TPTU Cornel Bupolo ameeleza kuwa lengo lao kuu kama chama ni kusaidia kupunguza baadhi ya migogoro ambayo imeonekana kuwa kero kwa upande wa walimu hao hasa changamoto za ndani ambazo hawana sehemu ya kuzifikisha.

“Tuligundua migogoro mingi inatoka nje sana, na tukaona kuruhusu masuala kama haya ingekuwa shida ndani ya nchi yetu,” amesema Bupolo.

Bupolo amesema  kazi yao kubwa nikusaidia walimu wote kwa ujumla ili wapate maslai yao kama inavyostahili kwasababu ni njia nyepesi ya kuifikishia serikali taarifa zinazo wakabili walimu.