Mawakala wanaodai fedha usajili wa simu wadhibitiwe

31Dec 2019
Mhariri
Nipashe
Mawakala wanaodai fedha usajili wa simu wadhibitiwe

Serikali iliweka wazi ma[ema wkamba usajili wa laini za siku kwa njia ya vidole gumba unafanyika bila malipo yoyote.

Kwa maana hiyo kampuni zote za simu za mkononi pamoja na mawakala wake wanapaswa kutekeleza kazi hiyo bila kudai malipo yoyote kutoka kwa wateja wa kampuni hizo.

Pamoja na maelekezo hayo ya serikali, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa ikisisitiza kuwa sharti pekee katia usajili wa simu ni mmiliki wa laoni ya siku kuwa na kitambulisho cha taifa ambacho hutolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida).

Hayo ndiyo maelekezo ya serikali tangu kuanza kwa usajili wa laini za simu kuanzia Mei mwaka huu, na hayajabadilika hadi sasa.

Hata hivyo, kutokna na baadhi ya wamiliki wa laini za simu kuchelewa kupata vitambulisho vya taifa au namba za vitambulisho hivyo, hali hiyo ilisababisha wakati fulani msongamano wa kusajili laini za simu hususan katika maeneo ya vijijini.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya mawakala wa kampuni za simu wasio waadilifu wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuwatapeli wananchi kwa kuwaambia kuwa bila kutoa fedha, laini zao haziwezi kusajiliwa.

Tangazo la awali la serikali kuwa laini zote ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo leo zingezimwa, limewalazimisha wamiliki kadhaa wa laini hizo kutoa fedha wka mawakala kuepukana na kuwa waathirika wa kuzimiwa simu.

Pamoja na wananchi kujua kuwa isajili wa laini ni bure, lakini wamekuwa wakitoa fedha kwa matapeli hao badala ya kutoa taarifa kwa mamkala husika kama TCRA na Jeshi la Polisi.

Malalamiko kadhaa yamekuwa yakitolewa dhidi ya mawakala kudai fedha, lakini bila hatua kuchukuliwa dhidi yao kutokana na mamlaka husika kutipelekewa taarifa.

Malalamiko hayo yako maeneo mengi lakini kwa kutoa mfano mmoja ni baadhi ya wananchi wa wilaya za Siha na Hai, mkoani Kilimanjaro kulalamikia hatua ya mawakala wa makampuni ya simu za mkononi kuwatoza fedha wakati wa usajili wa laini zao za simu ili wasajiliwe kwa haraka.

Kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki hii, tangu Rais John Magufuli atangaze kuongeza siku 20 zaidi za kusajili laini hizo, inadaiwa kuwa baadhi ya mawakala mitaani wenye mashine za kielekroniki zinazotumiwa kusajili, wamegeuza zoezi hilo kuwa fursa ya kujipatia fedha.

Walisema wanashangazwa na vitendo hivyo kwa kuwa katika matangazo ya serikali walielezwa kuwa kusajili wa laini ni bure.

Mmoja wa wananchi alisema alikwenda kusajili laini zake mbili kwa mawakala wanaokaa chini ya miavuli ya makampuni ya simu, na baada ya kusajiliwa aliambiwa atoe shilingi 2,000 kwamba kila laini moja nilipaswa kulipa shilingi 1,000. Kwamba alopohoji, alijibiwa kama anataka kusajiliwa bure aende kwenye maduka ya makampuni yaliyopo Moshi Mjini.

Tunaviona vutendo vya mawakala hao kufanya watakavyo kwa kudai wananchi fedha za usajili wa laini za simu ni kuidhalilisha serikali ambayo imetangaza kuwa usajili huo ni bure.

Pamoja pongezi kwa Rais John Magufuli Desemba 27, kutangaza kuonfeza siku 20 zaidi za usajili wa laini kuanzia Januari mosi, 2020 hadi Januari 20, tunashauri mamlaka husika kuingilia kati kuwakamata na kuwaadabisha wanaowadai fedha wananchi kwa ajili ya kusajili laini.

Ikiwezekana kuzibana kampuni zao kuwafungia kufanya kazi hizo kwa niaba yao.

Habari Kubwa