Wavulana vinara kidato cha pili

10Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Wavulana vinara kidato cha pili

KATIKA matokeo ya kidato cha pili yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) wavulana wameongoza nafasi ya kwanza hadi ya tano kitaifa, huku mwanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya upimaji huo akiwa ni Stephen Mwanzalima kutoka Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Marian ya mkoani Pwani.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, aliitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam sambamba na ya upimaji wa darasa la nne na mtihni wa kidato cha nne.

Akitangaza matokeo ya kidato cha pili, alisema ya wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya 571,137 wenye matokeo ya upimaji wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Kwa mujibu wa Dk. Msonde, kati yao wasichana ni 270,750 sawa na asilimia 89.30 na wavulana ni 243,501 sawa na asilimia 90.88.

Dk. Msonde aliwataja wanafunzi wengine walioingia 10 bora kitaifa na shule na mikoa yao kwenye mabano ni Raimond Tewele (Marian Boysa, Pwani), Jovin Magulu (Marian Boys, Pwani), Julius Mwaka (Marian Boys, Pwani), Luis Osena  (Marian Boys, Pwani), Violeth Emmanuel (Precious Blood, Arusha), Raymond Miho (Marian Boys, Pwani), Anna Kajiba (Canossa, Dar es Salaam) na Ibrahim Mawala (Marian Boys, Pwani).

WASICHANA 10 BORA KITAIFA

Violeth Emmanuel (Precious Blood, Arusha), Anna Kajiba (Canossa, Dar es Salaam), Leila Nakapi (St. Monica Moshono Girls, Arusha), Doreen Pallangyo (Marian Girls, Pwani),  Marystella Lyimo (Precious Blood, Arusha), Cecilia Dickson (Canossa, Dar es Salaam), Esther Lugola (Canossa, Dar es Salaam), Irene Mbai (Precious Blood, Arusha), Daima Salum (Marian Girls, Pwani) na Hope Kitaluka (St. Joseph Millenium, Dar es Salaam).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA

Stephen Mwanzalima (Marian Boys, Pwani), Raymond Tewele Marian Boys, Pwani), Jovin Magulu (Marian Boys, Pwani), Julius Mwaka (Marian Boys, Pwani), Luis Osena (Marian Boys, Pwani), Raymond Miho (Marian Boys, Pwani), Emmanuel Mtyama (Marian Boys, Pwani), Ibrahim Mawala (Marian Boys, Pwani), Norshad Kipenzi (Tengeru Boys, Arusha) na Gabriel Temba (Libermann Boys (Dar es Salaam).

Dk. Msonde alitaja shule 10 bora kitaifa na idadi ya wanafunzi wake kwenye mabano ni St. Francis, Mbeya (92), Kemebos Kagera (68), Centennial Christian Seminary, Pwani (152), Thomas More Machrina, Dar es Salaam (49) na Bethel Sabs Girls, Iringa (83).

Zingine ni  St. Augustine-Tagaste, Dar es Salaam (163), Bright Future Girls, Dar es Salaam (119), Anwarite Girls, Kilimanjaro (82), Feza Girls, Dar es Salaam (64) na Canossa, Dar es Salaam (89).

Dk. Msonde alitaja shule 10 zilizoongoza ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo ni Sogesca (Simiyu), Nyangao (Lindi), Jamhuri (Dar es Salaam), Dr. Asha Rose Migiro (Kilimanjaro), Consolata (Iringa), Kilwa Islamic (Lindi), Tabora Girls (Tabora), Arusha Day (Arusha), Magazini (Ruvuma) na Ahmes (Pwani).

Kwa upande wa shule 10 zilizoshuka ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo ni Mbwego (Tanga), Kibirashi (Tanga), Feo Girls (Ruvuma), Nkama (Tanga), Mrike (Kilimanjaro), Kilindi (Tanga), Kasela (Tabora), Katoke-Lweru (Kagera), Jaila (Tanga) na Mama Maria Nyerere (Mara).

Dk. Msonde alitaja mikoa mitatu iliyofanya vizuri zaidi ni Arusha, Iringa na Kilimanjaro na mkoa wa Lindi ulioongoza ufaulu kwa kipindi hicho huku mikoa miwili ambayo ni Tabora na Mara iliyoshuka ufaulu.

Alisema halmashauri 10 zilizofanya vizuri zaidi na idadi ya shule zake kwenye mabano ni Bagamoyo (21), Bukoba (30), Meru (60), Njombe (26), Morogoro 59 na Monduli (20).

Nyingine ni Kibaha (38), Moshi Mjini (23), Moshi Vijijini (94) na Arusha (51).

"Halmashauri 10 zilizoongeza ufaulu kwa miaka mitatu ni Meatu, Madaba, Newala, Arusha, Lindi, Siha, Ukerewe, Kibaha, Kiteto na Liwale," alisema.

Pia halmashauri 10 zilizoshuka ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo ni Kilindi, Mkuranga, Nzega, Kasulu, Buhigwe, Bukombe, Kigoma, Ulanga, Musoma na Serengeti.

Dk. Msonde alisema takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika masomo mengi ya msingi ambapo ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 50.28 na 92.19.

Aidha, alisema takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa wanafunzi hawakufanya vizuri katika masomo matatu ambayo ni Hesabu, Kemia na Historia.

Habari Kubwa