Fumbo linalowatesa Waingereza

15Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Fumbo linalowatesa Waingereza
  • wana - mfalme kuhamia uraiani
  • Mama Malkia: Basi tutafanyaje
  • Waziri Mkuu: Tuendelee kujadili
  • Wenye wafurahia kuhamia Canada

NDOTO ya mwanamfalme Harry na mkewe Meghan, kutaka kujiondoa katika maisha ya kifalme, imeanza kuleta mwanga mpya baada ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, kukubali ombi lao hilo.

Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan PICHA: MTANDAO.

Maisha ya wanandoa hayo yatakuwa katika nchi mbili za Canada na Uingereza katika kipindi cha mpito, wakati mchakato wa kujitoa ukiendelea.

Ni jambo lililoleta mshituko kuanzia kwa ndugu na jamaa zao na hata njeya jamii yao, hasa ikimaanisha Waingereza ikendana na swali ‘kuna nini?’

Hata hivyo kuna suala la ulinzi waio ambalo ni la lazima, nalo linabaki na swali itakuwaje? Kuna hasa kipengele cha ulinzi wao na gharama zake, watakapokuwa katika maisha mapya nchini Canada.

Ni jambo lililobaki tete, kiasi kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau, ametaka lijadiliwe, huku akiongeza inaenda mbali hata kwenye gharama za ulinzi wao huko ughaibuni utagharimiwaje?

Kupitia kikao kilichofanyika Jumatatu iliyopita, Malkia Elizabeth, amekubali kuwepo kipindi cha mpito wakati mwanamfalme Harry na mkewe Meghan, watakuwa wakiishi Canada na Uingereza.

Pia, Malkia Elizabeth anaunga mkono hatua yao kuanza kujitegemea, lakini anashauri kwamba ingekuwa vyema zaidi iwapo wangeendelea kutekeleza majukumu yao ya kifalme kwa muda.

Katika taarifa baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwenye makazi ya Malkia Norfolk, Jumatatu iliyopita, ambayo ilihusisha wanamfalme waandamizi, Malkia alisema anatarajia kwamba uamuzi wa mwisho utafanyika hivi karibuni.

Hatua hiyo imeibua maswali mengi ndani na nje ya ufalme wakihoji nani atawajibika kuwalinda na vyanzo vya kuwapatia mapato vitakuwa nini?

Trudeau anasema, raia wengi wa Canada wanaunga mkono hatua ya Harry na Meghan kuishi huko, lakini bado majadiliano zaidi yanahitaji kufanyika kuhusu gharama zilizopo.

Anaongeza kwamba hadi sasa serikali ya Canada bado haijahusishwa kuhusu kitakachohitajika katika hatua ya wanandoa kuishi nchini humo.

"Bila shaka tunaunga mkono hatua yao, lakini pia kuna wajibu wa kufanywa vilevile," anasema Malkia, katika mazungumzo yaliyomhusisha wanamfalme wa Charles na William.

"Japo tungependa wangeendelea kutekeleza majukumu yao ya kifalme kikamilifu, tunaheshimu na kuelewa matakwa yao ya kuishi maisha ya kujitegemea kama familia, wakiendelea kuwa sehemu muhimu ya familia yangu,” anasema.

“Tumekubaliana kuwa watakuwa na kipindi cha mpito ambapo wawili hao wataishi Canada na Uingereza baada ya Harry na Meghan kuweka wazi hawataki kutegemea pesa za umma katika maisha yao mapya," anasema Malkia Elizabeth.

Ni mazungumzo ya dharura yaliyopangwa baada ya Harry na Meghan kutoa taarifa iliyoishangaza familia ya kifalme wiki iliyopita, hatua kuzua kizungumkuti.

Hivi karibuni, Harrry na Meghan, waliibua mjadala mkali, baada ya kuzungumzia changamoto za maisha ya kifalme, ikiwamo hofu yao kuandamwa na vyombo vya habari.

Alionyesha wasiwasi wake huenda mkewe akakutana na yale ambayo mama yake Princess Diana alikutana nayo, hata kusababisha kifo chake.

MALKIA ANAJUTIA

Pamoja na uamuzi huo kutoka okoo wa kifalme, Malkia anaonekana dhahiri kujutia hatua ya Harry na Meghan kuwa huru na ndio maana, anataka waendelee kuwa na majukumu yao ya sasa.

Lakini, anajipa moyo kwa kueleza wao bado ni watoto wa kifalme na kwamba wataendelea kuthaminiwa wakati wanaendelea kujitegemea.

Inaonekana, Malkia anachukua hatua hii kama mchakato wa awali na wala siyo jambo la kumalizwa kwa siku moja na ndio maana anazungumza wapo katika kipindi cha mpito, huku suluhu yake haiwezi kupatikana ‘kesho’ wala miezi michache inayokuja.

Mkutano wa kujadili kujitoa mmoja wa wanamfalme ni wa kwanza kufanyika ndani ya himaya ya ufalme, baadhi ya Waingereza wanaona ni jambo lisilo la kawaida kulisikia.

MAOMBI YAO

Watu wengi wanaona mambo ya wanamfalme hao yanatokana na kuzidiwa na maisha ya kisasa, kwani tangazo lao walilitoa kipitia mtandao wa Instagram, jambo ambalo si la kawaida.

Meghan akiwa Canada na mtoto wake wa miezi nane na Archie, walifanya majadiliano hayo wakati wa Krismasi, kabla ya kurejea Uingereza kwa ajili ya majukumu ya kifalme.

RIPOTI ‘PORI’

Kumekuwapo ripoti kwamba ndugu hao wawili hawana uhusiano mzuri baada ya Willium kuonekana kuwanyanyasa wanandoa hao.

Hata hivyo, Harry na Willium, wamejitokeza haraka kukana madai hayo na kueleza taarifa hizo zimewaumiza kama ndugu.

Hata hivyo kwa mujibu wa chomho kimoja cha habari, ujnadaiwa mwanamfalme huyo alikuwa amekasirishwa na nduguye kuhusu mahojiano aliofanya na wanahabari.

Chanzo kingine kutika nyumba ya kifalme, kilisema kuluikwapo sababu tofauti ndani ya jengo la kifalme.

Kwa msaada wa mtandao

Habari Kubwa