Uturuki, Russia zaua vita za Libya na Syria

15Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Uturuki, Russia zaua vita za Libya na Syria

HATIMAYE kuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais Tayyep Erdogan wa Uturuki na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin mjini Ankara, Jumatano kusutisha mapigano katika nchi za ugenini nchini Libya.

Viongozi hao ambao kila mmoja anaunga upande mwingine, pia walikubaliana kusitisha mapigano nchini Syria na akatoa wito pande zinazogombana kuanza mazungumzo katika nchi zote mbili.

Ilikiwa ni sherehe nchini Libya kusikika wanasherehekea tangazo la kiongozi wa Jeshi la Taifa la Libya, la LNA, Jenerali aliyeasi Khalifa Haftar, kwamba anasitisha mapigano magharibi ya nchi yao, kuanzia Jumapili iliyopita.

Awali, Jenrrali Haftar, alipinga makubaliano hayo ya kusitisha mapigano lakini alibadili msimamo wake Jumamosi.

Msemaji wa LNA, Ahmed Mismari, alitangaza uamuzi huo kwa masharti kwamba upande wa pili unaheshimu mkataba huo.

Mismari anasema: “Uongozi wa Jeshi la Taifa la Libya, unatangaza usitishaji mashambulizi magharibi ya nchi kuanzia usiku wa manane wa Januari 12, 2020.”

AIitamka kwamba hilo linafanyika kwa sharti kwamba, upande wa pili unatekeleza usitishaji mapigano wakati huo huo na ukiukaji wowote wa makubaliano hayo, yatajibiwa vikali.”

Siku ya Jumapili iliyopita, Rais Erdogan amekuwa na mazungumzo mjini na Fayez al-Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali inayoitambuliwa na Umoja wa Mataifa, ambayo anaiunga mkono.

Jeshi linaloongozwa na haftar, lililoanza mashambulizi makali ya kuuteka mji mkuu wa Tripoli Aprili 4, inasaidiwa na Russia, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Huko Syria nako, usitishaji mapigano unatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumapili, ingawa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Syrian Observatory for Human Rights, linalofuatia vita huko, linaripoti vifo.

Kwa mujibu wa shirika linaripoti kwamba watu 17 waliuawa Jumamosi iliyopita, na wengine 40 walijeruhiwa baada ya Jeshi la Anga Syria kushambulia miji minne katika Jimbo la Kaskazini Magharibi la Idlib.

Haijajulikana bado, ikiwa serikali ya Damuscus inayoungwa mkono na Russia na Iran, itaheshimu makubaliano hayo.

Harakati za kusitisha mapigano Libya na Syria, zimekuwa zikifanyika wiki nzima kati ya nchi za Ulaya na Mashariki ya Kati, ambao viongozi wa mataifa mbalimbali wamekuwa wakikutana na pande zinazozozana katika nchi hizo mbili.

Siku ya Ijumaa iliyoishia, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, alitangaza kutakuwapo na mkutano wa amani wa Libya mjini Berlin, Ujerumani hivi karibuni baada ya kukutana na Rais Putin mjini Moscow, Russia.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, nalo liliidhinisha siku ya Ijumaa kuongeza muda wa kupeleka msaada wa dharura nchini Syria, ikiwa pia kuelekea jimbo la upinzani la Idlib.

Kwa mujibu wa taarifa za kimataifa.

Habari Kubwa