Unakijua kijiji? Hivi ndivyo kinavyojipanga, kufanya kazi

15Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Unakijua kijiji? Hivi ndivyo kinavyojipanga, kufanya kazi

UNAPOZUNGUMZIA msamiati kijiji, si mgeni kwa jamii. Mara moja kuna dhana ya kwanza inayojengeka, eneo lenye makazi ya pamoja ya watu, katika eneo lisilo mjini.

Katika zama za utekelezaji wa siasa za kijamaa, katika zama hasa kati ya mwaka 1964 na 1985, ilitumika sana kutekeleza uchumi kupitia itikadi za siasa hizo. Hapo ndipo kulizaliwa vijiji vya ujamaa na vijiji vya kawaida.

Kijiji kwa muundo na utekelezaji ndio unaunda serikali, ikiwa ndiko kwenye msingi mkuu wa serikali ya mtaa.

Mwaka 1975, panakumbukwa nchi kuwepo operesheni vijiji kitaifa, ambavyo katika sehemu nyingi watu walihamishwa makazi kuishi katika maeneo ambako serikali iliona ni bora kuwaletea maendeleo ya pamoja.

Makazi mapya yalianzishwa wakati huo, ikiwemo hata Jiji la Dar es Salaam, maeneo ya pembezoni kama Tegeta (Wilaya Kinondoni), Kubugumo na Mwanadilatu, ambako sasa ni jiji, kulikuwa vijiji vipya

MUUNDO WAKE

Kijijini ndiko kwenye maisha ya umma, wananchi wanashiriki katika serikali za mitaa au mikutano mbalimbali kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu mipango na matatizo yanayowakabili kurahisisha uboreshaji huduma za kijamii wanakoishi.

Huko ndiko asilimia kubwa ya wananchi wanapatikana, wengi wadau pacha wa uchumi; kilimo, ufugaji uvuvi.

Katika majukumu yao, mkutano wa kijiji ni chombo kikuu cha utawala na kipo kisheria. Wajumbe wake ni wanakijiji waliofikia umri usiopungua miaka 18 na hakuna akidi maalum ya kikao, ingawa kila kijiji hujiwekea, mathalani asilimia 20 ya wajumbe.

Kwa kawaida mkutano hufanyika kila baada ya miezi mitatu na kikao cha dharura kinaweza kuitishwa kukiwapo haja na kufanya hivyo. Taarifa ya kuitishwa Mkutano Mkuu wa Kijiji hutolewa si chini ya siku saba.

Pia, kila baada ya miaka mitano, kunakuwapo na mkutano mkuu maalum wa, uakindaa mchakato kwa wanakijiji kugombea nafasi za uongozi kwenye halmashauri ya kijiji au uenyekiti wa kijiji na nafasi nyingine kijijini.

Katika kuandaa mkutano, Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) hupanga ratiba za vikao na kuitisha vikao vya Mkutano Mkuu wa Kijiji.

MADARAKA MKUTANO

Kusimamia na kuwajibisha watendaji.

Kuweka taratibu za kuitisha vikao vya dharura.

Kupitia mkutano mkuu maalum wa uchaguzi. Kuchagua mwenyekiti wa kijiji na wajumbe halmashauri ya kijiji.

Kujaza nafasi wazi za viongozi wa halmashauri ya kijiji.

Kujadili na kupokea au kukataa taarifa za utekelezaji wa shughuli za kijiji kutoka halmashauri ya kijiji.

Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za kijiji.

Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa mapendekezo ya kodi, ushuru na vyanzo vingine vya mapato ya kijiji.

Kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya fedha za kodi, ushuru na mapato mengine kijijini.

Kupokea, kujadili na kufanyia uamuzi mapendekezo ya serikali ya kijiji kutunga sheria ndogo.

Kupokea, kujadili na kufanyia uamuzi ugawaji wa ardhi na matumizi ya rasilimali za kijiji.

Kuhoji, kudadisi, kukosoa, kukubali au kukataa taarifa na mapendekezo ya serikali ya kijiji.

Kuondoa madaraka serikali ya kijiji au mjumbe yeyote kabla ya muda wao.

Kupitisha azimio la kukaripia rasmi mjumbe yoyote wa halmashauri au halmashauri kwa ujumla kwa utendaji mbovu.

HALMASHAURI KIJIJI

Halmashauri ni chombo kikuu cha utendaji katika utawala wa kijiji. Hukutana mara moja kila mwezi na mikutano ya dharura inaweza kuitishwa, akidi yake ni nusu ya wajumbe wote kijijini.

Wakati Mkutano Mkuu ni kama Bunge, Halmshauri ya Kijiji ni kama serikali. Wajumbe wake huchaguliwa na mkutano mkuu wa kijiji, wakisimamiwa na mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya .

Ni mkutano mkuu, ambao kwa kushirikiana na mamlaka za kusimamia uchaguzi, hupendekeza idadi ya wajumbe wanaowafaa, kutegemea na wingi na ukubwa wa eneo lao (idadi ya vitongoji).

Humo kuna wajumbe kama mwenyekiti kijij, na wenyeviti kitongoji, viti vya wanawake wateule, halmashauri ikiongozwa na mwenyekiti wa kijiji, wanaochaguliwa na wakazi wa vitongoji husika

Katika majukumu yake, ndio injini ya kutafakari uamuzi, mapendekezo na maazimio ya mkutano mkuu wa kijiji na kubuni mbinu na njia za utekelezaji.

Ikiwa wajumbe wa halmashauri hawaridhiki na utendaji wa mwenyekiti wa kijiji, wana nguvu za kuendesha mchakato wakumuondoa na kuitisha mkutano mkuu wa kijiji, kuchagua mwingine.

Aidha, ndicho kikao kinachopekea taarifa za mikutano ya vitongoji na kamati zake, kufanyia kazi na kupeleka kwenye mkutano mkuu wa kijiji.

Lingine, ni upokea, kutafakari na kufanyia kazi maagizo na mapendekezo kutoka kamati ya maendeleo ya kata (WDC) na halmshari ya wilaya.

Halmashauri inabuni na kuendeleza sera na mwelekeo wa kijiji kwa mkutano mkuu wa kijiji, huku ikiandaa na kupendekeza mipango ya maendeleo ya muda mrefu kwa mkutano mkuu wa kijiji.

Pia inaweza kutunga sheria ndogo kwa kushauriana na mkutano mkuu wa kijiji, ikawaalika wataalamu panapokuwa na haja ya kufanya hivyo (ila hawatakuwa na haki ya kupiga kura).

Halmashauri ya Kijiji, inapokea, kutafakari na kupendekeza kwa mkutano mkuu wa kijiji, maombi ya ugawaji wa ardhi kubwa na ndogo, kumiliki mali na kuingia mikataba kwa niaba ya kijiji.

Kwa mujibu wa marejeo ya kitaalamu kuhusu muundo huo