Ubaguzi watu wenye ualbino washikiwa bango

20Jan 2020
Marco Maduhu
Nipashe
Ubaguzi watu wenye ualbino washikiwa bango

Shirika la Under the same sun kwa kushirikiana na mashirika wenza GNRC na CEFA wamezindua mradi wa “HAKI  YETU” awamu ya pili, ambao umelenga kupunguza ama kutokomeza kabisa matukio ya kikatili na ubaguzi ambayo wamekuwa wakifanyiwa watu wenye ualbino.

Uzinduzi wa mradi huo umefanyika jana Januari 19, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na viongozi wa kidini, ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimwakilisha Mkuu wa Mkoa Zainab Telack.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko mwenye nguo nyekundu katikati akikata utepe kuzindua mradi wa 'HAKI YETU' Kutoka Shirika la Under the Same Sun, ambao utatekelezwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya watu wenye ualbino, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Under The Same Sun, Berthasia Ladislaus na kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashidi Mfaume akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo Albert Msovela.

Akizungumza mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa mradi huo, amesema Serikali ina ahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili mradi huo upate kufanikiwa kwa asilimia 100, pamoja na kutoa elimu ya kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino, kuwaimarishia ulinzi na usalama, kuwapatia hifadhi na elimu katika shule ya Buhanghija Jumuishi, pamoja na kufanya msako kwa wale wote wanaotekeleza mauaji na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Mkurugenzi wa Under the same sun Berthasia Ladislaus akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa 'HAKI YETU'.

Meneja mradi wa 'HAKI YETU' kutoka Shirika la Under the same sun Wakyo Musong'o akielezea jinsia mradi utakavyokuwa ukitekelezwa mkoani Shinyanga.

 

Watoto wenye ualbino wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa HAKI YET, ambao unatekelezwa na shirika la Under the same sun ambao umelenga kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya watu wenye ualbino mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo wa HAKI YETU.

Habari Kubwa