Bilionea Mzimbabwe amaliza mgomo wa madakari kwao

24Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Bilionea Mzimbabwe amaliza mgomo wa madakari kwao

MADAKTARI nchini hapa wamekubali kurejea kazini, kwa kumaliza mgomo uliodumu kwa zaidi ya miezi minne.

Madaktari wa Zimbabwe walipoandamana. PICHA: MTANDAO.

Mgomo huo unaingia katika rekodi iliyodumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo na umeathiri vibaya mno sekta ya afya Zimbabwe.

Madaktari hao wamekubali kurejea kazini baada ya bilionea raia Zimbabwe anayeishi Uingereza, Strive Masiyiwa, kufikia makubaliano nao kuwa

kuwa atamlipa kila mmoja wao marupurupu ya takriban dola za Zimbabwe kwa mwezi za usafiri kwenda kazini, kupitia mfuko wa hazina utakaoanzishwa kushughulikia hilo.

Madktari wengi waliokuwa katika mgomo, wanapata mshahara chini ya dola 100 kwa mwezi. Bilionea huyo atagharamia mahitaji hayo ya madaktari kwa miezi sita. Haijabainika wazi ni kipi kitafuata baada ya kipindi hicho.

Ni mgomo ulioanza mwezi Septemba mwaka jana, baada ya kushindwa kufikia makubaliano na serikali ya Zimbabwe, madaktari zaidi ya 200 walifukuzwa kazi kwa kosa la kufanya mgomo.

Madaktari waliofutwa kazi, walikutwa na hatia ya kutokuwapo kazini, bila ya likizo wala sababu muhimu' kwa siku tano zaidi kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Huduma za Afya (HSB)

Madaktari hao wamekuwa wakidai malipo mazuri ya mishahara na ni mgomo uliosababisha kuzorota huduma katika hospitali kubwa, ambazo huduma za dharura pekee ndizo zimekuwa zikitolewa.

Msemaji wa Chama cha Madaktari nchini humo, Dk. Tawanda Zvakada, anasema ni miezi mitano anaingia hospitali bila kutoa huduma.

'' Nilipoingia kwenye wodi ya hospitali kwa mara ya kwanza, nilikuwa na hisia mchanganyiko. Nimefurahi kurejea, lakini hakukuwa na vifaa vya kutosha kwetu sisi kutoa huduma bora'', amesema Zvakada.

Kwa mujibu wa Dk. Zvakada, hali ilikuwa ya kuridhisha kwa sababu madaktari wamerejea, wodi zimefunguliwa na sehemu za kuona madaktari zilizofungwa, sasa zimefunguliwa tena.

Madaktari wanasema kwamba, walitaka suluhu ya kudumu lakini hawakuweza kufikia makubaliano na serikali na kurudi kwao sasa kumetokana na makubaliano na asasi inayoongozwa na tajiri huyo.

''Watu wamepoteza maisha, wengine wamepata ulemavu ambao hauwezi kurekebishika,'' anasema Dk. Zvakada.

Aidha, madaktari hao wanaeleza matumaini kwamba watafikia makubaliano ya kudumu na serikali, wakitoa na wito wa kuangaliwa kwa madai yao ambayo hayajabadilika.BBC

Habari Kubwa