Virusi vya corona

25Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Virusi vya corona
  • *Vyayumbisha dunia kupata tiba, kinga
  • *Kujikinga kwa ‘maski’ puani waibua utata

MATAIFA ya Afrika mashariki yametangaza kuchukua hatua ya tahadhari kukabiliana na virusi vya Corona vinavyosababisha maradhi ya homa kali ya mapafu.

Raia wa China akiwa amejikinga dhidi ya virusi vya Corona kwa kutumia kitambaa cha puani

Mtu akipata virusi hivyo anakuwa na homa kali ambayo anashidwa kupumua na wakati mwingine husababisha kifo.

Mpaka sasa idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa virusi hivyo nchini China imeongezeka na kufikia 26.

Afrika Mshariki ikiwamo Tanzania ni mshirika mkuu wa kibiashara  na  China,  maelfu ya raia wa nchi hiyo wanaingia kila siku kufanya kazi mbalimbali ikiwamo kutalii.

Kenya, Uganda na Tanzania zimeanza kuchukua hatua kwa kutoa tahadhari na kufanya uchunguzi abiria wanaowasili katika mataifa hayo..

Maofisa wa China wanasema mpaka juzi kuna visa vipya 830 vya maambukizi ya virusi hivyo vimethibitishwa.

Wataalamu kutoka shirika la Afya Duniani wamesema ni mapema kutangaza mlipuko wa virusi vya Corona kuwa janga la kimataifa.

Kufikia sasa karibu miji 10 katika mkoa wa kati nchini China ambayo ina watu milioni 60 imewekewa vikwazo vya usafiri ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo.

Mataifa mengine yalioathiriwa na virusi hivyo ni Vietnam na Singapore, Thailand, Japan, Taiwan, Korea Kusini na Marekani.

NINI NJIA SAHIHI KUJILINDA?

Uvaaji wa kitambaa puani inaelezwa ndio njia sahihi ya kukabiliana na virusi hivyo, na katika nchi zilizothibitisha kukumbwa na tatizo hilo wanashauri watu wake kuvaa pale wanapotoka ndani.

Kitambaa hicho cha kuziba mdomo ambacho ni maarufu katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya kujizuia maambukizi, kinatumika sana China huku watu wakipewa ushauri wa kuejiepusha na mahali palipo na msongamano wa watu.

Wataalamu wa afya wameelezea namna kutumia kifaa hicho ili kuzuia virusi.

Kitambaa cha puani kilianza kutumika kwa mara ya kwanza katika hospitali mwishoni mwa karne ya 18, lakini zilikuwa hazitumiki katika sehemu za umma mpaka mlipuko wa mafua ulipotokea Uhispania.

Dkt David Carrington, kutoka chuo kikuu cha St George, mjini London, Uingereza,  aliiambia BBC kuwa ‘Maski’ zinazotumika wakati wa operesheni au upasuaji huwa haziwezi kufanya kazi vizuri katika maeneo ya umma.

Anasema kitambaa cha aina hiyo hakiwezi kufanya kazi vizuri dhidi ya virusi vya bakteria wa hewa ambao wanaambukiza, kwa sababu zina nafasi za wazi na zinaacha macho wazi.

Lakini zinaweza kupunguza maambukizi kwa kiasi fulani ya kuwakinga watu katika maambukizi ya mkono na mdomo.

Utafiti uliofanywa kutoka New south Wales, ulipendekeza kuwa watu huwa wanashika nyuso zao mara 23 kwa saa.

Profesa Jonathan Ball, kutoka chuo kikuu cha Nottingham, anasema kuwa katika utafiti mmoja uliofanywa hospitalini, unaonesha ‘maski’ ya sura huwa nzuri kwa kuzuia maambukizi kama ilivyobuniwa.

Wabunifu waliotengeneza kifaa hicho kwa namna ambayo inaweza kuzuia vimelea vya hewani.

Ingawa  ukiangalia ufanisi wake kwa ujumla katika msongamano wa watu, takwimu zinaonyesha utofauti mdogo.

“Vilevile si rahisi kwa mtu kukaa na kifaa hicho kwa muda mrefu ," Prof Ball aliongeza.

Dkt Connor Bamford, wa taasisi ya afya ya Wellcome-Wolfson, iliyopo chuo kikuu cha Queen Belfast, anaeleza kuwa kuweka mazingira safi ni hatua rahisi na nzuri kwa kinga.

"Utekelezaji wa kuweka mazingira safi ndio hatua rahisi zaidi ambayo inaweza kufanya kazi kwa uhakika". anasema

Hata hivyo, China yathibitisha kwamba virusi vya Corona vinaweza kusambazwa kwa njia ya hewa.

“Kuziba mdomo wakati unapiga chafya, kunawa mikono, na kujizuia kuziba midomo kwa mikono kabla ya kunawa, kunaweza kupunguza hatari ya maambukizi kupata virusi", anasema.

Dkt Jake Dunning, mkuu wa masuala ya afya nchini Uingereza anatilia shaka kifaa hicho akisema "Ingawa kuna watu wanahisi kuvaa maski usoni kutasaidia watu kupata maambukizi, kuna ushahidi mdogo sana kuwa kitendea kazi hicho kinaweza kuwanufaisha watu wakiwa nje kwa sababu imebuniwa kwa ajili ya huduma za afya,” anasema.

Anasema maski hizo kama hazikuvaliwa vizuri, kubadilishwa kila wakati kunaweza kuwa salama  katika mazingira ya kazi.

Watu wangezingatia zaidi kufanya mazingira yao kuwa safi, kama hilo suala la usafi wangelipa kipaumbele, anasisitiza Dkt. Dunning.

Kwa msaada wa BBC

Habari Kubwa