Elimu duni, uzembe chanzo kikubwa janga ajali pikipiki

20Dec 2019
Yasmine Protace
Nipashe
Muungwana Lazima Nilonge
Elimu duni, uzembe chanzo kikubwa janga ajali pikipiki

USAFIRI wa bodaboda upo takribani kila kona ya nchni na umekuwa ukitumiwa na watu mbalimbali.

Hata hivyo, kuna baadhi ya maeneo ambako bodaboda hizo zilianza mbali zaidi, nikiutaja mkoa jirani wa Kagera, hasa mjini Bukoba.

Usafiri wa bodaboda umekuwa ukitumiwa na watu mbalimbali ukiwawezesha watu kufika kwa urahisi katika maeneo waendayo, kwani hayapotezi muda katika foleni, hasa katika maeneo ya mijini.

Usafiri huo, pia umekuwa ukitumiwa na baadhi ya wazazi kwa kuwapeleka watoto shule, kutokana na wengi kushindwa kulipia usafiri wa mabasi ya shule.

Katika kufuatilia, nimebaini jambo moja kwamba, madereva wanaoendesha bodaboda, wengi hawana elimu inayojiteshekeza kwa ajili ya kutumia vyombo hivyo.

Serikali imekuwa ikizungumzia hilo kila mara, kwamba kila anayetumia usafiri wa aina yoyote, ni lazima azingatie sheria, itakayomuwezesha kufika safari yake salama, katika sehemu aendayo
.
Kuna baadhi ya watu wanaovunja sheria kupitia vyombo vyao na wanapokamatwa, wanajihisi sheria imewaonea, wakati katika ukweli si sahihi, bali inakuwa kinyume chake.

Mtu anapoambiwa anapoanza safari yake, baadhi ya mambo ya msingi kama vile kufunga mkanda ni ya kuzungatia.

Pia, hata wale wenye watoto wanatakiwa wawaweke katika viti vyao, lengo ni kuwanusuru na uwezekano wa madhara safarini, hasa pale ajili inapotokea.

Lakini, mtu akiangaliwa katika magari binafsi, baadhi yake hazizingatii hilo, watoto hayo wanakalishwa kwenye viti vya mbele na hawana vizuizi vyovyote.

Hapo ni kwa ajili ikitokea mtoto kupona ni shida.
Ukija upande wa bodaboda ambao nauzungumzia ni kila bodaboda ibebe abiria mmoja na kuwapo kofia ngumu mbili za dereva na abiria wake

Lakini, cha kushangaza unakuta baadhi ya bodaboda hawazingatii hilo na kuamua kufanya watakavyo wao.

Unakuta abiria wapo watatu katika bodaboda na aliyevaa kofia ngumu ni dereva pekee je ajili inapotokea nani wa kulaumiwa.

Kwa nini dheria tunazivunja wenyewe,wakati tunajua bodaboda moja inabeba mtu mmoja? Tujue, bila ya
kufuata saheria za usalama barabarani, bodaboda zitaendelea kusumbua na kuifanya serikali iingie gharama kubwa kuhudumia majeruhi ikiwamo matumizi makubwa ya damu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Limataifa Masuala ya Usalama Barabarani, Fotunatusi Sokoni, anatoa mfano ajali za pikipiki kwa miaka miwili tofauti, zilisababisha jumla ya vifo 2,953.

Anaainisha, mwaka 1997 zilisababisha vifo vya watu 990 na majeruhi 1,997; huku mwaka 2017 kulitokea 1,584 zilizosababisha vifo 763 na majeruhi 1,224.

“Ukiangalia mwaka 2016 na 2017 kuna tofauti ya ajali 1,019, yaani zilipungua kwa kiwango cha asilimia 22.9 na waliojeruhi ilikuwa ni pungufu ya watu 773 katika kipindi hicho,” anasema.