Imekuwaje Mchina katushinda Kwenye mtihani wa Kiswahili?

25Feb 2016
Gwamaka Alipipi
Nipashe
Muungwana Lazima Nilonge
Imekuwaje Mchina katushinda Kwenye mtihani wa Kiswahili?

WAKATI Watanzania wakiona lugha za kigeni kama Kichina, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani ni kigumu kujifunza kwa kusoma kuandika ma kuhesbu, maarufu kama KKK, mwanafunzi raia wa China, Congcong Wang, amewadhihirishia Watanzania kuwa hakuna kinachoshindikana katika kujifunza lugha ya taifa fulani.

Imeonekana maajabu katika sekta ya elimu nchini, kwa raia wa kigeni kuongoza kitaifa na somo la Kiswahili amepata daraja ‘B’ huku wazawa wakianguka kwa kupata alama ambazo si za kupendeza.

Nadhani hata nchi za jirani ambako wamesikia habari hiyo, watakuwa wanajiuliza swali imekuwaje, Waswahili wameshindwa na Mchina katika kuandika na kusoma Kiswahili, hata Kiingereza ambacho kwa Mchina ni lugha ya mbali kwake.

Katika mikusanyiko ya baadhi ya watu, mitandao ya kijamii hasa Facebook, Instagram na WhatsApp jina la Congcong, ndilo lililochukua nafasi kubwa ya mijadala mbalimbali.

Wadau wengi wamekuwaa wakiuliza ,amewezaje kushika nafasi hiyo na hasa kupata alama ya juu katika somo la Kiswahili wakati si lugha yake?

Kwa waliowahi kusoma masomo ya lugha katika elimu ya sekondarim watakubalina nami kuwa mtihani wa somo la Kiswahili umegawanyika katika sehemu kadhaa kama vile Insha, Matumizi ya lugha, Fasihi na Sarufi.

Ni dhahiri mwanafunzi huyo aliweza kusoma maswali yote yaliyokuwa katika karatasi mtihani wake wa Kiswahili na kuyaelewa vizuri, hata akayajibu kwa kuandika kwa ufasaha.

Swali linajitokeza tena, inakuwa vipi kwa wanafunzi wa Kitanzania wanakwama kujifunza lugha za mataifa mengine, hususan katika sekta ya elimu hadi inafika hatua ya kukwama katika ambayo wana asuili nayo?

Je, ni kutokuwa na walimu wenye ujuzi wa kufundisha masomo hayo ya kigeni au ni mazingira ya ufundishaji? Tunajikuta wanafunzi wa Kitanzania wanayakimbia masomo kama Kifaransa kwa madai kuwa ni magumu.

Nilimsikia Congcong akihojiwa na waandishi wa habari. Alisema sababu ya kufanya vizuri katika somo la Kiswahili ni juhudi kubwa aliyofanya katika kukijua Kiswahili.

Pia alisema kwamba, alitamani sana kufaulu somo la Kiswahili, hali iliyomfafanya ajifunze lugha hiyo kwa bidii. Katika mtihani wake, masomo yote alipata alama, lakini Kiswahili pekee pekee ndilo somo alilopata B.

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia mna Ufundi, inapaswa kupokea changamoto hiyo iliyoonyeshwa na raia wa kigeni kukijua Kiswahili, hata kujibu maswali ya mtihanio kwa ufasaha na akawashinda wazawa wan chi wenye lugha yao.

Hali hiyo imemaanisha inawezekana kwa wanafunzi wa kitanzania kuweza kujua lugha za mataifa mengine kwa kusoma na kuandika vizuri, hali itakayosaidia kuongeza wataalam wa sekta mbalimbali nchini.

Serikali inapaswa kuweka misingi bora katika sekta ya elimu, ili kuwatengenezea wanafunzi mazingira rafiki ya kupenda kujifunza lugha za kigeni.

Ni aibu kubwa kwa serikali na wanafunzi wote wa Tanzania, kushindwa mtihani wa lugha ya taifa na raia wa nchi nyingine aliyeanza ‘A’ kujifunza lugha hiyo.

Leo tunashuhudia raia wa Kichina anaongoza somo la Kiswahili, hatuju kesho ni nani? Si ajabu tukasikia Mjerumani na keshokutwa akawa Mfaransa, wote walioongoza soko la Kiswahili, kisha wazawa tunadumu katika nafasi yetu ya kushika mkia katika somo ambalo asili yake ikio kwetu.

Nawapinga wanaosema masomo ya lugha za kigeni kama vile Kiingereza na Kifaransa ni magumu. Wapo wanaonda mbali zaidi, kwa kutamka kuwa “Kiingereza si lugha yetu na ndiyo maana tunaanguka.”

Wito wangu ni kwamba, wanafunzi walioko shuleni na hasa walioko katika shule za msingi na sekondari, waamini kwamba hakuna jambo linaloshindikana katika kujifunza, ili mradi wakiweka na katika kutafuta wanachokihitaji, watakipata.