Kisa cha wanasiasa na mamantilie

01Nov 2020
Nkwazi Mhango
Nipashe Jumapili
FIKRA MBADALA
Kisa cha wanasiasa na mamantilie

WANAOJUA historia ya wanasiasa kugeukana, hawatashangaa maneno ya hivi karibuni ya mwanasiasa mmoja kusema atampigia kura mgombea wa chama kingine na kumtosa mgombea waliyempitisha kwenye chama chao. Kimsingi, ameonyesha kile ambacho Waingereza huita verisimilitude; picha ya kweli na halisi.

Hii imenikumbusha kisa cha rafiki yangu. Alikwenda kwa mamantilie kupata mlo. Akiwa anangoja mlo, alisikia mamantilie akimtuma msaidizi wake kwenda kumnunulia chakula hotelini. Jamaa alishtuka kunani; akaamua kuondoka bila kuaga wala kungoja chakula. Maana yake nini? Mamanitilie alijua madawa machafu na sumu alivyokuwa akitumia kuvutia biashara.

Katika sakata hili kadhalika, kwa wanaojua ajenda binafsi na ithibati ya wahusika yaani ulaji, hawatashangaa wala kushuku maneno na msimamo aliouchukua mwanasiasa huyo.

Ajabu ya maajabu hata mwanasiasa mwingine (Mwenyekiti wa chama) ameamua kuukoleza kwa kukuza mgawanyiko akimuunga mkono mwenyeji wake asijue nani atafuata! Je, kinachojifunua hapa ni nini, mwisho wa mwanzo wa ndoa ya wanasiasa hao umeanza au ndo siasa? Je nani anatamchuuza mwenzake? Who’s hoodwinking whom? Waingereza huuliza. Kwa uzoefu wa uharibifu, mwanasiasa huyo ana kila sababu ya kuchekelea. .......kwa habari zaidi tufuatilie kupitia epaper.ippmedia.com