Mifuko plastiki imeondoka, vifungashio pia haviko sawa

07Jun 2019
Yasmine Protace
Nipashe
Muungwana Lazima Nilonge
Mifuko plastiki imeondoka, vifungashio pia haviko sawa

TAREHE Mosi iliyopita, ndio ulikuwa mwanzo wa marufuku kwa matumizi ya mifuko ya plastiki Tanzania Bara, ambayo sasa iko kisheria. Wenzetu Zanzibar wanayo muda mrefu.

Kutokana na kupigwa marufuku mifumo hiyo, serikali ilitoa matangazo na kutaka uwepo mifuko mbadala kwa ajili ya kubebea bidhaa hizo.

 

Hivyo basi, watu wamechangamkia fursa hizo kwa kutengeneza mifuko mbadala kama ilivyoagizwa na serikali.

Mifuko ya plastiki inajulikana kuwa na madhara makubwa kiafya. Inaelezwa hata ikifukiwa haiozi na panapofanyika kilimo cha mazao, nayo haiozi.

Vivyo hivyo, inapoliwa na mnyama, haisagiki katika mfumo wa mwili wa mwanadamu, nayo katika hatua hiyo anadhurika.

Tumeona katika mitandao ya kijamii, baadhi ya watu wamekuwa wakihamasisha watu kujiunga katika makundi, ili waweze kupata elimu ya kutengeneza mifuko mipya mdadala.

Kimsingi, tunapongeza juhudi hizo, kwani ni fursa ya kumuongezea mjasiriamali mdogo kipato cha ziada katika hilo.

Pamoja na kutengeneza kwa mifuko mbadala na kuinogesha kwa rangi maridhawa, tunaomba ubora uzingatiwe kutokana na pesa inayotumika kununua mfuko huo kubwa.

Bei mpya sasa ni kati ya Sh. 400 hadi Sh.1000, nasikitika kusema kupitia ushuhuda wa siku hizi chache tumegundua baadhi ya mifuko hifai, licha ya kuwa na rangi bora, japo ipo sokoni.

Unakuta mfuko unawekewa bidhaa, unachanika kabla ya kuanza safari. Sasa hapo ni kumtia hasara aliyenunua vitu.

Inatakiwa wazalishaji waboreshe mifumo yao ili kuunguze malalamiko ya wateja. Nimtetee muuzaji katika hilo, hana kosa ndani ya wiki hii moja ya biashara mpya. Tukisema kosa namkosaji, moja kwa moja lipo kiwandani kwa wazalishaji.

Hiyo ni kwa sababu, tena katika mwanzo huu hatujui wazalishaji mifuko hiyo walilenga mbebaji wa vitu gani, hata kufikia isichanike kirahisi.

Ukienda madukani, hata uthabiti wa mifuko hiyo ukiwekewa soda, basi hata chupa mbili huwezi kuuning’iniza. Inabidi uikumbatie, maana ukining’iniza, hufiki mbali na chupa hizo, lazima zitaanguka na kupasuka.

Tunayapenda mabadiliko haya. Ila wazalishaji wa mifuko hii mipya waache kulipua. Tutengenezeeni vile yenye  viwango.

Nihamie kwa marafiki zangu wa magengeni. Mnatumia bahasha za kuhifadhia pesa kuwekea wateja vitunguu na nyanya. Kweli huo ni mfuko mbadala?  Ni mazingira nayo mnatakiwa kujiongeza katika magenge yenu.

Haya, nao wale wauza chipsi mlo wa wakazi wa mjini na vijana. Unapouza foili au ‘take away’ sio kuwawekea wateja wa chips katika mifuko ya kaki au magazeti.

Unakuta mteja anawekewa chipsi zinamafuta alafu anawekewa katika mfuko wa kaki au gazeti kwa kiafya sio sahihi.

Wauza chipsi wanatakiwa kujiongeza kuna wateja ambao wanatoka maeneo ya hapo jirani hawa nirahisi kuwa na kifaa cha kubebea na kuna wapita njia hawa wamekuta chipsi na wanataka kuondoka nazo, eti unamfungia katika gazeti au unaweka katika mfuko wa kaki, hii haipendezi.

Top of Form

Bottom of Form