Riba kubwa mikopo ni kikwazo

22Sep 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mtazamo Yakinifu
Riba kubwa mikopo ni kikwazo

MIKOPO mingi ukiachia ile ya vichochoroni, hata baadhi ya mabenki yamekuwa yakitoza riba kubwa kiasi kwamba mwisho wa siku mtu unajikuta una zigo kubwa la kutua.

Kuna mabenki yanatoza riba kiasi kwamba unapopata fedha ile badala ya kuona unafuu
unajiona kama una mzigo mkubwa tena wa kuubeba.

Ingawaje kuna benki chache
zinazoweza kukopesha kwa riba kidogo tunadhani kuna haja ya kuangalia benki nyingine nazo zifanye hivyo.

Lengo la kutoa fursa ya mikopo ni kuwawezesha wananchi waweze kuongeza kipato chao,lakini kama mkopo huo utaanza kuonekana kuwa ni mzigo basi hata mkopo huo hautakuwa
na faida sana.

Tunaomba mamlaka husika ziangalie jinsi ya kurekebisha riba hiyo ili tuweze kunufaika.