Siku Trump alipoivua nguo Marekani

17Jan 2021
Nkwazi Mhango
Nipashe Jumapili
FIKRA MBADALA
Siku Trump alipoivua nguo Marekani

ZIKIWA zimesalia wiki mbili kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, anayemaliza muda wake, kuondoka Ikulu Jumba Jeupe (White House), hali ilichacha na kuchafuka kweli kweli. Mnamo Januari 6, 2021 ilikuwa “siku ya kiza” (rais mteule Joe Biden) na simanzi katika historia ya Marekani.

Kwani ni siku ambapo Rais wa Marekani alianzisha maasi dhidi ya taifa hili lenye kujivunia mizizi ya kidemokrasia huku likijiteua kuwa polisi wa demokrasia duniani.

Akiwa ameshindwa uchaguzi mkuu wa Novemba, 2020 na Biden, alikataa kumtambua, kumpongeza wala kukubali ushindi huu, Trump aliamua kufanya kile ambacho walatini huita sacriligo (sina tafsiri) au tuseme kilihataji kiasi fulani cha uchizi. Kutokana na hili, Wamarekani walitaka Trump aondolewe ofisini haraka ili Makamu wake wa Rais, Mike Pence amalizie ngwe yake.  Wengi wanajua namna Trump alivyohutubia mkutano wa hadhara muda mfupi kabla ya kuwahimiza wahuni na wabuguzi wa kimarekani kuvamia jengo la Bunge la Marekani la Capitol Hill na ‘kuirejesha nchi yao nchi yao’ wakati wabunge na maseneta wakiwa kwenye vikao vya kuhakiki na kupitisha ushindi wa Biden. 

Katika uvamizi huu, mtu mmoja alipigwa risasi na kufariki huku askari polisi akijeruhiwa na kufa baadaye hospitalini mbali na wengine wanne waliofariki kutokana na kukosa huduma za matibabu. Wahuni hawa walijitokeza wakiwa na bendera ya kibaguzi na ya ile yenye maandishi ya Trump.

Baada ya shambulizi hili la aibu na hatari, maseneta na wabunge walirejea Capitol Hill na kumaliza kupitisha ushindi wa Biden. Walivamia wakiwa chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais Pence huku usalama wake, familia yake na wabunge ukiwa hatarini.

Kituko ni kwamba, askari wa jiji la Washington na wengine wa vyombo vya usalama hawakuonekana kama walivyofanya wakati wa maandamano ya amani ya watu weusi ya Black Lives Matter kabla ambapo walijazana na kuwasambaratisha kwa mabomu ya machozi na pilipili na risasi za mpira....soma zaidi kupitia https://epaper.ippmedia.com