Sote tujiunge kupiga vita wasichana kutoa mimba

10Jan 2017
Halfani Chusi
Nipashe
Muungwana Lazima Nilonge
Sote tujiunge kupiga vita wasichana kutoa mimba

UTOAJI mimba, tafsiri yake rahisi ni kitendo ambacho mwanamke mjamzito anakatisha uhai wa kiumbe kipya tumboni mwake, kwa kuharibu mfumo wake na kiumbe hicho kinatoweka.

Suala hilo kwa sasa limekuwa endelevu hususan kwa wanafunzi shuleni, wamekuwa wakitoa mimba, ili waweze kuendelea na masomo, licha ya kuwa ni kati ya vitu vinavyopingwa vikali na taasisi tofauti nchini

Licha ya kupingwa vikali, bado utoaji mimba unaonekana nchini kuwa na madhara makubwa kwa jamii za Kitanzania.

Vifo, katika hatua ya kutoa mimba kifo ni asilimia 90, kwani katika hatua hiyo, mama mjamzito anapotoa mimba, hutokwa na damu nyingi inayomhatarisha hata uhai wake.

Mtu anayetoa mimba mara nyingi afya yake huendana na hali ya kuwa dhaifu na inamchukua muda, kurejea katika afya ya kawaida.
Anapokutana na hali hiyo, mtu huwa na mwili dhaifu ghafla, kwani anakuwa amepoteza damu nyingi.

Binafsi napinga sana tendo hilo kwani kwa kuingia kwa kina kiimani, inawezekana mtu anapotenda hilo, linakuwa katika mazingira yanayokinzana na maagizo yake, kwani inawezekana binadamu asijue amepangiwa kupata watoto wangapi.

Pia, katika maisha yetu ya kawaida binadamu, naona ni kupingana na sheria zilizowekwa na serikali yetu.

Kuna baadhi ya jamii, tena sasa ikiwa ajenda ya kimataifa, wakihimiza hivi sasa kusiwapo tabia ya kutolewa mimba, huku tabia hiyo kisiri inakuwa sugu.

Naomba kutoa ushauri kwamba, kama mtu amepatwa na mimba bila kutarajia, kamwe usithubutu kutoa mimba, kwani hakuna anayejua mtoto atakayezaliwa, nini itakuwa nafasi yake duniani.

Imani zetu zinatuambia kwamba “kila binadamu amekuja na riziki yake duniani.”

Pia, mama huyo katika afya yake utauweka mwili katika majanga makubwa na hatari ya kupatwa na magonjwa yanayotokana na upungufu wa damu mwilini

Vilevile, wazazi tuna jukumu la kujizuia dhidi ya hasira zitakazotutawala, mtoto atakaposhika mimba isiyotarajiwa kwa watoto wetu wengi wa kike, kwa inapowatokea, wanakuwa na hofu na mawazo ya kutoa mimba.

Nikiri kwanza kuwa ni tendo linalotia hasira sana, lakini nafasi ya uzazi unchukua nafasi.

Kuna wazazi ambao kutokana na sababu za kutokuelewa, mara nyingi wamekuwa ikisababisha watoto wao kutoa mimba, kutokana na hofu ya kukosa jibu la kuwapa wazazi wao pindi, watakapohijiwa namna walivyopata mimba hiyo.

Lakini pia serikali licha ya kukemea suala hili la utoaji mimba kupitia vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini pia ingeunda vikundi vitakavyo jihusisha na uelimishaji jamii juu ya madhara ya utoaji mimba na kuelimisha njia za kuepuka mimba zisizotarajiwa, ili kinamama wasikutane na adha ya utoaji mimba

Cha muhimu, wazazi wajitahidi kuwahimiza watoto wao kuwa tayari kukua katika maadili ya kidini, yanayochangia watoto wengi kuepuka mimba zisizotarajiwa.

Hata takwimu ziliozopo, zinaonyesha kuwa wanao kumbwa na matukio ya utoaji mimba, ni watoto walio katika umri mdogo, ambao kimsingi wapo chini ya malezi ya wazazi